Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza kwenye
mkutano na Kamati ya Wachimbaji na Wanunuzi wa Jasi na Makaa ya Mawe
Tanzania. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Dangote, nchini Tanzania, Harpreet Duggal akifuatiwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo, Devakumar Edwin.
Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo hivi karibuni alikutana na
wajumbe wa Kamati ya Wazalishaji na Wanunuzi wa Madini ya Jasi na Makaa
ya Mawe Nchini katika Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Masuala
mbalimbali kuhusiana na biashara ya madini hayo kwa ujumla yalijadiliwa
kwa lengo la kuleta tija kwa pande zote na Taifa kwa ujumla.
Mkutano
huo ulihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Wizara ambao wamo ndani ya
Kamati husika akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Madini na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa James
Mdoe, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje na Makamishna
Wasaidizi wa Madini kwenye Kanda zinazozalisha madini husika.
Kutoka
kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Madini ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati husika,
Profesa James Mdoe, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje na
Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin
Mchwampaka wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo (hayupo pichani).
Wawakilishi
kutoka Kampuni inayochimba Makaa ya Mawe ya Tancoal waliohudhuria
mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu, Jim Shedd, Mkuu wa
Masoko, Emmanuel Constantinides na Mkurugenzi Mtendaji, Mark McAndrew
wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
(hayupo pichani).
Baadhi ya
Wajumbe wa Kamati ya Wazalishaji (Wachimbaji) na Wanunuzi wa Madini ya
Jasi na Makaa ya Mawe waliohudhuria mkutano huo.
Baadhi ya
wajumbe kutoka Kampuni ya Dangote wakimsikiliza Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). Wa kwanza kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Dangote, Devakumar Edwin, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Dangote, nchini Tanzania, Harpreet Duggal.
Comments
Post a Comment