Miezi
takribani mitano iliyopita tangu aondolewe Billcanas, siku moja tangu
Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo katika shamba lake,
Mwenyekiti huyo wa Chadema amepewa siku 14 awe amelipa kodi
inayokadiriwa kufika milioni 13.5, ya hoteli yake ya Aishi iliyoko
Machame Mkoani Kilimanjaro.Uamuzi huo mpya wa Serikali wa Wilaya ya Hai,
Mkoani Kilimanjaro,umefikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Mkuu
wa Wilaya hiyo Gellasius Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za
kilimo katika shamba la Veggies analomiliki Mbowe kutokana na kile
kilichosema lipo ndani ya chanzo cha maji.Byakanwa amesema kuwa Serikali
ya awamu ya Tano imelenga kukusanya mapato ili iweze kutekeleza
majukumu yake ikiwamo kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi
(CCM).“Hatuwezi kufikia malengo ya ukusanyaji mapato yetu ya ndani kama
kuna wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na tena
kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo
yataweza kujulikana kiasi anachostahili kulipa kodi,”amesema Byakanwa.
Hata
hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amemshutumu Mbowe kwa kufanya uharibifu wa
mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha mkuu wa Wilaya
kulingana na uamuzi wa Kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta
maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa
maji mfereji.
CHANZO: MTANZANIA
Comments
Post a Comment