
Msemaji
wa Jeshi la Senegal Kanali Abdou Ndiaye amethibitisha kwamba vikosi
hivyo vimevuka mpaka na kupiga hatua kuelekea katika Mji Mkuu wa nchi
hiyo, Banjul na kusema kwamba vikosi hivyo mpaka sasa havijakabiliana na
ukinzani wa aina yoyote ingawa viliweka bayana kwamba vilikuwa
vimejizatiti kwa mapigano ikibidi.Mapema Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa inasemekana kwa siri limekuwa likiunga mkono juhudi za vikosi
vya ECOWAS, kuhakikisha kwamba rais Barrow anachukua madaraka kutoka kwa
rais aliyemaliza muda wake Yahya Jammeh. Rais huyo wa zamani wa Gambia,
awali aligoma kuachilia madaraka.Rais wa sasa Adama Barrow ameapishwa
leo katika nchini jirani kwenye ubalozi wa Gambia ulioko mjini Dakar
nchini Senegal na kufuatiwa na shamra shamra ubalozini hapo.
Mpaka
sasa haijafahamika wazi lini rais mpya wa Gambia ataweza kurejea nchini
mwake na kuchukua hatamu za uongozi kwa mara ya kwanza akiwa rais.
Comments
Post a Comment