CHECK PICHA RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP ALIPOANZA KUITUMIA NDEGE YA AIR FORCE ONE


Wiki moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump ameanza kuitumia ndege maalumu ya Rais “Air Force One” ambapo aliipanda kwa mara ya kwanza January 26, 2017 wakati akienda kuzungumza na Maseneta wa chama cha Republican huko Philadelphia.
Rais huyo ameikubali ndege hiyo na kuisifia kwa kuwa ni ya kisasa kuzidi ndege yake binafsi ambapo amenukuliwa akisema “Ni ndege nzuri, kubwa na ya kisasa kuzidi ndege yangu Boeing 757 japokuwa nayo ni nzuri lakini Air Force One ni zaidi”
Nimekuwekea hapa picha zikimuonesha Rais Trump akiwa kwenye ndege hiyo.
      

Comments