WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa ameugiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro (NCAA), kumpelekea nyaraka zote zilizotumika katika
kumuhamisha faru maarufu kwa jina la John katika hifadhi hiyo ifikapo
Desemba 8, 2016.
Ametoa
agizo hilo leo (Jumanne, Desemba 6, 2016) alipotembelea Ofisi za makao
makuu ya NCAA, zilizoko wilayani Ngorongoro mkoa Arusha wakati
akizungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa Baraza la
Wafugaji ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani hapa.
"Nina
taarifa zenu kuwa mlimuhamisha kwa siri faru John kreta na kumpeleka V I
P Grumet Serengeti Disemba 17, 2015 na mliahidiwa kupewa sh. milioni
200 ambapo mkapewa sh. milioni 100 kwa ahadi ya kumaliziwa sh. milioni
100 nyingine baadaye,".
“Naomba
niletewe nyaraka zote zilizotumika kumuomba na kumuondoa faru huyo na
barua zilizotumika kujadili suala la faru John. Nasikia amekufa naomba
pembe ziletwe ofisini na iwapo itathibitika aliondoka bila ya kufuata
taratibu wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria,”.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu apega marufuku tabia ya baadhi ya watumishi
wa mamlaka hiyo ambao wanawakabidhi watoto kupeleka ng’ombe wao ndani ya
kreta. “ Watumishi wa Ngorongoro ndiyo wanaopeleka ng’ombe ndani ya
kreta na si wenyeji. Sasa marufuku na tutakayemkuta hatutakuwa na
msamaha naye,”.
Amewataka
watumishi hao kuhakikisha wanakuwa waadilifu na wanafanyakazi kwa
kufuata misingi ya kiutumishi na kuacha tabia za kuendekeza rushwa na
wizi.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa NCAA, Sezzary
Simfukwe kutokana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili na
tayari anahojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU).
"Haiwezekani
mtumishi awe anachunguzwa na TAKUKURU halafu aendelee kuwa ofisini si
atavuruga uchunguzi. Asimamishwe kazi kuanzia leo mpaka hapo uchunguzi
utakapokamilika na aikibainika kwamba hana hatia atarudi kazini,”
alisema.
Pia
Waziri Mkuu alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa NCAA, Fred Manongi kueleza
zilipo sh. bilioni moja zilizotolewa na Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya
Kikwete kwa ajili ya kujengea ranchi ya wafugaji wa tarafa ya
Ngorongoro.
Akijibu
swali hilo Manongi alisema wakati Rais Kikwete anatoa fedha hizo alikuwa
bado hajateuliwa kushika washifa huo, ambapo Waziri Mkuu alimuagiza
Mkurugenzi huyo kufanya uchunguzi juu ya fedha hizo na kasha kumpelekea
tarifa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Comments
Post a Comment