Wananchi wa Kata ya Lyambamgongo-Bukombe wamvutia Mbunge wao katika shughuli za maendeleo.

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akisaini kwenye kitabu cha wageni mara tu baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Lyambamgongo kwa ajili ya kujionea shughuli zilizo fanywa wananchi kwa kujitolea wenyewe.
 
  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko wakiwa na Diwani wa Kata ya Lyambamgongo Mhe. Shitobelo(mwenye tisheti nyeupe) pamoja na wadau wengine kwa pamoja wakiangalia hatua zilizo fikiwa kwa sasa na wananchi wa Kata hiyo ya Lyambamgongo katika ujenzi wa Kituo Cha Afya kwa kujitolea kwa nguvu za zao bila shuruti baada ya kuteseka kwa mda mrefu wa kuishi bila kupata huduma hiyo ya Afya kweye Kata hiyo.


Hizi ni tofali zilizoandaliwa kwa nguvu za wananchi ili kujenga Kituo cha Afya kwenye Kata ya Lyambamgongo.

 Ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb)  alifika katika eneo hili lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya msingi Ifunde na haya ni mawe yaliyosombwa kwa nguvu za wananchi wa Kijiji cha Ifunde ili waweze kujipatia shule yao wenyewe na kuwapunguzia umbali watoto wao wanaokwenda kutafuta elimu katika Vijiji vingene vya jirani.
 
 Haya ni matofali yaliyofyatuliwa kwa nguvu za wananchi wa Kijiji cha Ifunde ili waweze kujipatia Shule.
 
 Picha ya  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na Diwani wa Kata ya Lyambamgongo Mhe. Shitobelo(wa katikati),Katibu wa Mbunge Jimbo la Bukombe Bw. Benjamini Mgeta(mwisho kulia) na Fundi aliyehusika katika ujenzi wa Kisima hicho kwa pamoja wakiangulia hatua zilizofikiwa katika ujezi huo wa kisima kinachotegemewa na vijiji takribani vinne ikiwa baadhi ya vijiji hivyo ni Uzunguni,Ishololo,Bukombe na Lyambamgongo yenyewe. 

 

Comments