MHE DOTO AFANYA UZINDUZI WA KIKUNDI CHA AMANI-NTENGERE

Wanakikundi wa Amani wakimpokea kwa shangwe kubwa  Mbunge wao Mhe. Doto Mshaka Biteko baada ya kuwafikia kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa kikundi hicho.

 Baadhi ya wanakikundi wakitumbuiza Nyimbo.
 Mwenyekiti wa CCM Tawi la Ntengele na mlezi wa Kikundi cha Amani akisoma risala kwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.

 Picha ya baadhi ya wageni waalikwa katika uzinduzi huo wa Kikundi cha Amani.
 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akipokea keki kutoka kwa wana kikundi wa Amani


 Diwani wa Kata ya Bulangwa Mhe. Yusuph Mhamed akizungumza na wanakikundi wa Amani 

 Diwani viti maalum(CCM) akiwapongeza wanakikundi hao kwa maamuzi walioyafanya ya kuamua kuungana na kutengeeza Kikundi na waahidi kuwachangia elfu Hamsini kwa ajili ya kutunisha mfuko wa kikundi hicho.

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akikata keki.

 Mmoja wa wanakikundi akila keki kwa Tsh elfu ishirini kwa ili kuinua mfuko wa Kikundi hicho cha Amani.

 Mwenyekiti wa CCM Tawi la Ntengele na mlezi wa Kikundi cha Amani nae akitoa pesa Tsh. elfu thelathini ili kutunisha mfuko wa kikundi hicho. 


 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akitoa Pesa Shilingi Laki Tano Taslimu ili kutunisha mfuko huo wa Kikundi cha wamama wajasliamali kinachoitwa Amani- Ntengere.


 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wanakikundi hao wa Amani alisema huu ni wakati wa kufanya kazi hivyo asitokee mtu hata mmoja wa kuwakatisha tamaa na kuwasihi kuendelea kushikamana na kushirikiana kwa karibu zaidi hususani kutembeleana na kushauliana mambo mazuri yenye kuleta maendeleo bila kujali itikadi dini wa ukabila. 

Comments