Msanii
mkongwe wa nyimbo za Injili nchini Rose Muhando amekanusha taarifa
ambazo zilizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa ameingia katika
matumizi ya Madawa ya kulevya.Muimbaji
huyo alidai taarifa hizo zilisambazwa na watu ambao hawamtakii mema
katika maisha yake kutokana na kwenda nao tofauti katika makubaliano ya
kufanya nao kazi.
“Situmii
madawa na sitatumia, kama waliona ndiyo skendo itakayonimaliza
wameshindwa, wanaofanya hivyo ni watu wanaotaka kunimaliza walitaka
nifanye kazi zao, nikakataa.” Rose aliuambiia mtandao wa gazeti la
Mwanaspoti.
Aliongeza,
“Sijajiingiza na mambo hayo na wanavyozungumza nasikitika kwa sababu
wanaiumiza familia yangu kisaikolojia, mimi ni mama wa watoto watatu na
nina ndugu zangu, naambiwa mambo yote hayo kwa sababu sina mtu wa
kunitetea,”
Katika katua nyingine muimbaji huyo alizungumzia kuhusu ukimya wake pamoja na ujio wake mpya.
“Nipo
hata hivyo kuna kazi nyingine nimeandaa ipo kwa Alex Msama bado
haijatoka kutokana na mambo mbalimbali, ingawa naandaa kazi nyingine
ninayotegemea kuikamilisha mwezi wa tatu mwakani tutakapojaaliwa.
Nimeshaanza kuandaa baadhi ya nyimbo na nyingine naendelea kutunga,
unajua kazi hizi huwa nasikiliza sauti ya Mungu aniambie niimbe nini.”
“Pia,
nimekuwa nafanya huduma ya kuimba katika mikutano tofauti ndani na nje
ya nchi kama hivi jana umenikuta natoka kijiji cha jirani kuimba na wiki
iliyopita, nilikuwa Kenya ambako nilifanya huduma, Kisumu na Mombasa,
nimeamua kufanya hivyo kwa sababu zangu,” anasema Rose.
Comments
Post a Comment