Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 5,678 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, wafungwa 1,340 wataachiwa huru
na 4,338 watatumikia kifungo kilichobaki baada ya kupunguziwa moja kwa
sita ya vifungo vyao.
Rais ametoa msamaha huo kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45 (1) (d) ya Katiba.
Rwegasira
imeeleza kuwa wafungwa wote wamepunguziwa vifungo vyao zaidi ya punguzo
la kawaida linalotolewa chini ya kifungu 49(1) cha sheria ya Magereza
sura ya 58.
Amesema
wafungwa waliopewa msamaha huo ni pamoja na wagonjwa wa Ukimwi, Kifua
Kikuu (TB) na saratani na ambao wamethibitishwa na Jopo la Waganga chini
ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au wa Wilaya.
Comments
Post a Comment