Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari akionesha baadhi ya vifaa
walivyokutwa navyo majambazi hao ikiwemo silaha.Askari wa Jeshi la
Polisi Mkoani Mbeya wamefanikiwa kuzuia tukio la ujambazi katika
mapambano ya kurushiana risasi na watu waliosadikiwa kuwa ni majambazi
na kuua wawili kati yao.Taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari imesema kuwa mnamo tarehe 19.12.2016
majira ya saa 1:45 jioni katika Kijiji cha Busisya, Wilaya ya Rungwe,
Askari Polisi walipata taarifa za siri za kuwepo kwa majambazi wenye
silaha ambao walikuwa na lengo la kufanya uvamizi katika Duka la
Mfanyabiashara wa soda na bia za jumla ambaye pia ni wakala wa kutuma na
kupokea pesa kwa njia ya mtandao.
Askari
hao walianza kuwafuatilia majambazi hao na muda wa saa 1:45 jioni askari
walikutana na majambazi hao wakiwa wamepakiana katika pikipiki ambapo
baada ya majambazi hao kugundua kuwa wanafuatiliwa na askari walianza
kuwarushia risasi askari na ndipo yalitokea majibizano ya risasi kati ya
askari na majambazi hao.
Askari
walifanikiwa kuwapiga risasi majambazi wawili ambao walifariki papo hapo
na mmoja wao aliweza kutupa silaha aliyokuwa akiitumia na kukimbia.
Pia baada
ya kupekuliwa majambazi hao walikutwa na vitu vingine ambavyo ni Rungu
moja, Praizi moja, Bisibisi moja, mafuta ya cherehani, koti la ngozi
rangi ya brown pamoja na begi dogo rangi nyeusi ambalo lilitumika
kuhifadhi vitu hivyo.
Comments
Post a Comment