Mbunge Doto aungana na wanakikundi cha Hekima kujichotea baraka kwa watu wasiojiweza


Picha ya baadhi ya wanakikundi pamoja na wadau wanaosaidia na kikundi hicho cha Hekima wakiwa katika Hafla hiyo fupi Ofisini kwao. 

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko wakati  akizungumza na wanakikundi hao alianza kwa kuwapongeza kwa hatua walizozichukua za kupambana na ukatili dhidi ya mama mtoto sambasamba na kuwawezesha watu wanao ishi katika mazingira magumu hasa wajane,wazee na walemavu kwa kuwapa misaada hiyo ya chakula,mavazi pamoja na kuwatembelea mara kwa mara katika makazi yao huku akiwasihi wanakikundi hao wa Hekima kutokatishwa tamaa na mtu yeyote kwani kutoa ni baraka na wajiandae kulipwa na MUNGU na kuogeza kuwa hakuna aliyetoa kwa moyo na asichote baraka.
Pia Mhe. Doto wakati akitoa misaada hiyo iliyo andaliwa wanakikundi wa Hekima aliunguna nao kuchota baraka hizo kwa kuwawezesha mitaji ya biashara walezi wa watoto huo ili waweze kufanya biashara na kujipatia kipato ili waweze kujikimu na kuepukana na hali ya kuomba misaada mara kwa mara hatima kuwa mjasilia mali mzuri.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akifanya zoezi la utoaji  misaada iliyoandaliwa na wanakikundi wa Hekima.

Picha ya Pamoja baada ya zoezi hilo.

Comments