Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko ameongoza mamia ya wananchi wa Kata ya Ushirombo katika Mazishi ya mama mmoja aliyeuawa kikatili
Wakirejea nyumbani baada ya shughuli ya kustili.
Diwani wa Kata ya
Ushirombo Mhe. Lameck Warangi akitoa pole.
Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wanandugu wa karibu wa marehemu Bi Sofia Mlimandoke.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko ameongoza mamia ya wananchi wa Kata ya Ushirombo - Bukombe, Mkoani Geita
kuuaga mwili wa mama mmoja(Bi Sofia Mlimandoke)
aliyeuawa kinyama kwa kukatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana.
Akizungumza katika tukio hilo, Mhe. Doto
ametoa pole kwa familia ya marehemu na wananchi wote kwa ujumla .“Tumepokea
taarifa za msiba wa mama huyu kwa
mshtuko mkubwa sana kwani sio kifo cha kwaida kwa mwanadamu katoa uhai wa
mwenzake,” amesema.
Amesema wafiwa wanatakiwa kuishi kwa upendo na kumshirikisha Mungu ili kuepusha uhasama ndani ya familia zao . “ Tuiombee familia iwe na moyo wa utulivu katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.”
Amesema wafiwa wanatakiwa kuishi kwa upendo na kumshirikisha Mungu ili kuepusha uhasama ndani ya familia zao . “ Tuiombee familia iwe na moyo wa utulivu katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.”
Pia aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa karibu na kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya wilaya ili kuhakikisha watu hao waovu wanatiwa mbaroni.
Nae Diwani wa Kata ya
Ushirombo Mhe. Lameck Warangi wakati akitoa pole kwa wananchi wa Kata yake
amesema kila mwananchi anawajibu wa kuwa mlinzi ili kuhakikisha tukio kama hilo halijirudii
tena.
Comments
Post a Comment