Tukio la
kushangaza lililohusishwa na kifo cha Denis Komba (24) baada ya nyoka
aliyekuwa naye kuuawa, limechukua sura mpya baada ya mambo kadhaa
kuibuka.
Hayo ni
pamoja na familia kudai mzoga wa nyoka na kwenda nao kuuzika nyumbani,
jambo lililoendelea kuhusisha suala hilo na imani za kishirikina.
Imeelezwa
kuwa familia ilielezwa na mganga wa kienyeji kuwa mwili uliohifadhiwa
hospitali, si wa mtoto wao, jambo lililowafanya kuuchukua mzoga wa nyoka
na kwenda kuuweka katika mfuko wa sarandusi (kiroba) na kuuzika.
Hata
hivyo, mashuhuda walieleza kuwa, familia hiyo ilikikata kichwa cha nyoka
na kukizika kivyake na kiwiliwili sehemu nyingine huku mwili wa Komba
ambaye naye alizikwa jana, ukizikwa katika kaburi eneo lingine tofauti.
Tukio hilo ni la juzi na lilimhusu Komba, mkazi wa Mateka, manispaa ya
Songea mkoani Ruvuma.
Nyumbani
kwao ni kilometa tano kutoka katikati ya mji wa Songea. Kabla ya maziko,
baadhi ya vijana waliokuwa wamebeba jeneza, walikuwa wakikimbia nalo
mwendo wa mchakamchaka huku wakiimba “mkimbize mkimbize nyoka awahi
asije kudhuru watu wengine”.
Katika
maziko hayo, hakuna ndugu aliyeonekana kulia wala hakukuwa na ibada
yoyote wakati jina la marehemu linadhihirisha kuwa ni wa imani ya
Kikristo. Wakati hayo yakiendelea msibani, baadhi ya watu wake wa karibu
walidai alikuwa na tabia ya kucheza na nyoka mara kwa mara.
Hata
hivyo, baba mzazi alikana kumuona mwanawe na nyoka. Naye daktari
aliyechunguza mwili, alisema kifo cha Komba kinatokana na kugongwa na
nyoka mwenye sumu kali, lakini hakuna jeraha wala alama yoyote
iliyoonekana katika mwili huo.
Source: Habari Leo
Comments
Post a Comment