Timu zikielekea waliko wasimamizi wa mchezo tayari kwa ukaguzi na
wenye jezi nyekundu ni Timu ya Eleven King Fc na waliobaki ni Wachezaji wa Timu ya Rufuna Fc.
Mwamuzi wa ndani ikifanya utambulisho kwa viongozi wa Chama cha mpira Wilaya ya Bukombe (BUFA),na mwenye Shati nyeupe ni Katibu BUFA bw. Bosco Mwidadi anafuata ni Mtunza Hazina wa BUFA bw. James Malima.
Mashabiki kama kawaida yao
Timu ya Rufuna Fc iliyoko Kata ya Katente Wilayani Bukombe Mkoani Geita
jana imejinyakulia ushindi wa gori 1-0 dhidi
ya Timu ya Eleven King Fc iliyoko Kata ya Bulega kwenye ufunguzi wa ligi daraja
la nne inayosimamiwa na Chama cha Mpira Wilaya Bukombe (BUFA)iliyoanza jana katika
viwanja vya Bulega .
Mechi hiyo iliyohudhuliwa na mamia ya mashabiki katika uwanja
wa Bulega Timu ya Rufuna Fc iliichapa gori 1 bila Timu ya Eleven King Fc dakika
ya 43 kupitia kwa kiungo mshambuliaji Nestor
Jamhuli.
Hadi dakika tisini ya mchezo huo Timu ya Eleven King fc haikupata hata gori la
kufutia machozi.
wakati akizungumza katibu wa chama cha mpira wilaya ya
Bukombe Bw. Bosco kwenye ufunguzi wa
ligi hiyo aliwaeleza wachezaji na
mashabiki kuwa lengo la ligi hiyo ni kukuza vipaji vya vijana kimichezo hivyo haina
haja ya ugomvi ndani na nje ya uwanja huku akiwasihi wananchi wa Bukombe na
viunga vyake kujitokeza kwa wingi kutazama ligi hiyo ili kuwatia hamasa vijana
wanao shiriki katika ligi hiyo.
Kwa upande wake kocha
wa timu ya Rufuna Fc bw. Benjamini Rufuna Ntoro
amewashukuru wachezaji wake kwa ushindi walioupata na kuwataka kuendelea
kufanya mazoezi kwa bidii ili
kufika waendelee kufanya vizuri katika mechi ijayo ya marudiano na kujichukulia ushindi tena.
Nae katibu wa timu ya Eleven King bw. Nestory Machibya aliyapokea matokeo hayo
ya kushindwa na kuwataka wachezaji hao kutokata tamaa kulingana na kushindwa
kufikia malengo yao.
Comments
Post a Comment