Halmashauri kuu ya CCM-Bukombe yapewa taarifa ya utendaji ya miezi sita 2016

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi-Bukombe Mhe. Zacharia Bwire (katikati) kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Josephat Maganga na kushoto kwake ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe Michael Bundala mwishoni ni Katibu Msaidizi Ngwanda na mwenye sutu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bukombe Bw. Dionis Myinga kwa pamoja wakiimba kabla ya kuketi na kuanza kikao cha Halmashauri kuu ya CCM-Bukombe. 

Picha ya baadhi ya wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM-Bukombe wakiwa tayari kwa kusikiliza taarifa ya Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa yaliyojili na utekelezaji wake tangu Julai-Desemba 2016 iliwa ni dusturi yake kwa kila baada ya miezi sita kutoa taarifa ka hiyo.
Timu ya wataalaum wakiwa wamejumuika katika mkutano huo wa halmashauri kuu ya CCM-Bukombe.
 
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko wa kwanza kushoto anaefuata ni katibu wa Madiwani na Diwani wa Kata ya Igulwa Mhe. Richard Mabenga akiwa na wajumbe wengine katika Mkutano huo wa Halmashauli kuu ya CCM-Bukombe.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe Michael Bundala akiwamesimama kwa aijili ya utambulisho.
Makatibu wa Jumuiya mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Bukombe wakiwa katika umakini wa kusikiliza.


Na Taarifa ya yailiyojili na utendaji wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Dto Mashaka Biteko  tangu Julai-Desemba 2016 ameitoa kama ifuatavyo;

Kiambatisho NA1

ZIARA YA MBUNGE WA JIMBO LA BUKOMBE KUANZIA TAREHE 19.07.2016
NUSU YA PILI YA MWAKA WA KWANZA

TAREHE
KATA
MAHALI MKUTANO ULIPOFANYIKIA

JUMLA YA MASWALI NA VIPENGELE VYAKE
YALIYOJITOKEZA
19/07/2016
RUNZEWE  MAGHARIBI
KIJIJI CHA MSANGILA
60
·         Kituo cha Afya
·         Maji
·         Kucheleweshewa kwa pembejeo za kilimo.
·         Kupata soko la udaga.
·         Barabara kuunganisha vijiji
·         TASAF kuna changamoto.
·         Upungufu wa nyumba za walimu.
·         Mahusiano mabaya kati ya wananchi na wahifadhi.
·         Elimu itolewe juu ya wajasiriamali.
·         Wafugaji wapewe Eneo la Malisho.

20/07/2016
KATOME
KIJIJI CHA BUGAMA
15
·         Huduma ya Afya hafifu.
·         Mzani wa LULA badala ya Digital.
·         Dawa ya pamba feki.
·         Wakulima kukatwa fedha kwenye zao la pamba.
·         Baraza la Madiwani liwe na Mwakilishi toka kundi la walemavu.
20/07/2016
IGULWA
KIJIJI CHA BUNTUBILI
42
·         Wafugaji kutengewa Eneo la kuchungia.
·         Ushuru mdogo mdogo bado upo.
·         Dawa feki ya pamba.
·         Manyanyaso kwa wananchi juu ya wahifadhi.
·         Ukosefu wa Dawa Hospitali ya (W).
·         TASAF Igulwa hakuna.
·         Upimaji wa Mji Kata Igulwa.
·         Uchimbaji mdogomdogo wa madini.
·         Maji.
·         Kujenga Sekondari Igulwa.
·         S/Msingi Buntubiri walimu watoke saa 8:30 Mchana.
·         Kiwanda cha kusindika Asali.
·         Chuo cha Veta.
·         S/Msingi Igulwa kupewa mifuko  ya CEMENT 20 (MB)


27/07/2016
LYAMBAMGONGO
KIJIJI CHA LYAMBAMGONGO
44
·         Nyakumbu secondary wanafunzi wana changishwa Tsh: 450,000/=
·         Shule zenye ufaulu mzuri zawadi.
·         Maji katika S/Msingi.
·         Kituo cha Afya.
·         Wanafunzi kuacha shule.
·         Kipimo cha Mozambique.
·         Umeme kupitia kando rami.
·         Mbegu ya pamba feki na dawa feki.
·         Nyumba za walimu.
·         Mizanani ya digital inawaibia
·         Barabara
·         Gari la wagonjwa Lyambamgongo
28/07/2016
BUSONZO
KIJIJI CHA NAMPALAHARA GENGENI
38
·         VEO Nampalahara kunyanyasa wananchi.
·         Mzani wakulima wanahitaji wa rula.
·         TASAF fedha zinazotolewa ni kidogo mf 40,000 kwa familia kubwa.
·         Maeneo ya wachimbaji wadogo wadogo.
·         Sekondari ya Busonzo ifunguliwe.
·         Maji ya kisima kirefu.
·         Mgonjwa wa kansa atibiwa.
·         Mnada wa Busonzo asilimia wanapata kikundi kidogo badala ya Kata.
·         Kituo cha Afya hakuna kwenye kata hii.
·         S/Msingi Gengeni Mbuge Msaada kusaidia ujenzi CEMENT Mifumo 50.

02/08/2016
BULANGWA
USHIROMBO SEKONDARI
46
·         Walimu waliosimamia mtihani kidato IV 2015 hawakulipwa.
·         Walimu wa sayansi ni wachache sana.
·         Walimu hawana vitambulisho.
·         Walimu wapya hawana mshahara.
·         Madai ya walimu bado kunachangamoto.
·         Watoto wa shule kukaa kumbi za video.
·         Walimu wapewe motisha.
·         Umeme haujasambazwa vya kutosha
·         Upungufu samani za Ofisi .
·         Michango ya vyeti vya mgambo.
·         Mashirika mbalimbali yasaidie Elimu.
·         Mchango ushirombo sekondari 2,700,000/=kwenye mfuko wa waalimu (Mb)
04/08/2016
KATENTE
HOSPITAL YA (W)
42
·         Kazi za Fedha zitokanazo na mfuko wa Jimbo.
·         Umeme kutosambaa pote.
·         Waandishi wa habari kutoa  taarifa za uongo.
·         Clinic ya baba, Mama na watoto ni ndogo sana.
·         Maji hakuna.
·         Chumba cha upasuaji hakina ubora.
·         Madai ya watumishi.
·         Ultrasound iliyopo haitoshi.
·         Uhaba wa watumishi.
·         Zabuni za majengo yote Hospital watumishi washirikishwe.
·         Kichomea taka hakifanyi kazi.
·         Watumishi kupandishwa vyeo.
04/08/2016
USHIROMBO
KIJIJI CHA BUSINDA
24
·         Barabara.
·         UMWAPA unakata  Pamba.
·         Pembejeo zifike muda mwafaka.
·         TASAF inachangamoto.
·         Kituo cha Afya.
·         Matibabu ya jino yamepanda sana.
·         Msindikwa wapate shule.
·         Umeme.
·         Maji.
05/08/2016
RUNZEWE MASHARIKI
KIJIJI CHA BULUMBAGA
6
·         Wafugaji kulisha shamba na kumpiga mwenye shamba.
·         MWL Mkuu kuwa na mgogoro
·         Vifaa vya michezo.
09/10/2016
BUGELENGA
BUFANKA
27
·         Kuto kamilika Zahanati ya Bufanka.
·         Choo cha S/Msingi Bufanka kutokamilika.
·         Upungufu wa madawati S/Msing .
·         Maji ya visima virefu.
·         Wakulima waliokatwa pembejeo warudishiwe gharama zao.
·         TASAF inachangamoto kubwa sana.
·         Vituo cha Afya msasani lini kitaanza kazi.
·         Milioni Hamsini zitapatikana lini.
·         Elimu bure ukomo wake juu ya wananchi.

10/10/2016
BULEGA
KIJIJI CHA KAKOYOYO
40
·         Pesheni kwa wazee.
·         Barabara toka kakoyoyo hadi Butinzya.
·         Azimio kiwe Kijiji.
·         Wakulima wakikatwa zao la pamba.
·         Maeneo ya malisho ya mifugo.
·         TASAF na changamoto.
·         Milioni Hamsini.
·         Uhitaji wa Chuo cha Veta Bukombe.
·         Upungufu wa walimu.
·         Maji.
·         Mtu mwenye bima akanunue dawa.
·         Upungufu wa madawati.
·         Walemavu na wajane wasaidiwe.
·         Wahudumu vijiji wapate baiskeli.
11/10/2016
UYOVU
S/MSINGI KAPWANI
13
·         Kupata vifaa vya michezo.
·         Kupandishwa kwa Madaraja.
·         Kwa walimu na Mishahara  yao.
·         Fedha za mfuko wa Jimbo kujenga choo cha S/Msingi Kapwani.
·         Doto CUP washerikishwe Netball .
·         Walimu kufanya kazi kwenye Mazingira magumu.
·         Walimu walioajiriwa 2013 hawa kulipwa.
·         Kituo cha michezo (W) Bukombe kipo S/Msingi Kapwani.
11/10/2016
UYOVU
WACHUNGAJI WOTE TARAFA YA SILOKA

·         Maeneo ya wachimbaji.
·         Upungufu wa Madarasa.
·         Upungufu wa vitu vya Afya na Zahanati.
·         Wachungaji Ofisi za Serikali wana bezwa na viongozi.
·         Mahakama ya mwanzo Msasa imekithiri rushwa
·          Kituo cha Afya Uyovu kina upungufu wa dawa.
·         Wazee vikongwe kukoswa matibabu.
·         Baadhi ya wanasiasa wanapotosha Umma.
·         TASAF bado inachanga moto.
·         Ukosefu wa S/Msingi Masambi kunachangia watoto kugongwa gari.
·         Makanisa baadhi yao wanazuiliwa kikesha.
12/10/2016
NAMONGE
MJI MWEMA
39
·         S/Msingi Mji Mwema watoto kutofundisha.
·         Barabara toka Bugege, Mji mwema ichakaya hadi Namalandula.
·         Eneo la mifugo kuchungia.
·         Mwaka huu Pembejeo zipatikane mbegu bora na dawa zake.
·         S/Msingi Mji Mwema walimu kutokukaa shuleni.
·         Zahanati kila kijiji.
·         Maji.
·         Manyanyaso toka kwa wahifadhi.
·         Kituo cha Afya Namonge.
·         Veo Mji mwema kutokukaa Ofisini .
·         Zao la Tumbaku kuna mgogoro.
·         Milioni Hamsini zinakuja lini.
·         Pesheni kwa wazee.
·         Umeme.
·         Pembejeo hufika nje na wakati.
·         Umeme bado sana Bukombe.
04/11/2016
MHE  MBUNGE
UYOVU NA BUSONZO
KUKAGUA MIRADI
·         Ujenzi wa vyumba vya madarasa na choo Ibamba S/Msingi.
·         Barabara toka Uyovu hadi Busonzo
05/11/2016
IGULWA
KIJIJI CHA KAPELA
26
·         Barabara za mitaa Igulwa.
·         Maji.
·         Umeme.
·         Milioni Hamsini.
·         Kupata Eneo la kuchimba wa chimbaji wadogo wadogo.
06/11/2016
UYOVU
KIJIJI CHA AZIMIO

·         Azimio hakuna S/Msingi
·         Ushuru mdogo mdogo bado unatozwa
·         Mgogoro wa kisiasa Azimio
·         Eneo la kuchimba wachimbaji wadogo wadogo
18/11/2016
NAMONGE
KIJIJI CHA NAMONGE, Mhe. Mbunge,madiwani na Kamati ya maafa ya Wilaya walitembelea wahanga walioathirika na mvua iliyoambatana upepo
FARAJA NA MSAADA
·         Ghala la Tumbaku
·         S/Msingi Namonge madarasa 3
·         Baadhi ya nyumba za wananchi
·         Nyumba za Ibada kuezuliwa
·         Mhe. Mbunge alitoa msaada kwa baadhi ya waathirika hasa wajane na wasiojiweza kabisa pamoja na makanisa

01/12/2016
BULEGA
Kijiji cha Bulega
Mbunge kushirikiana  na wananchi
·         Kujitolea kusomba mawe kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa S/M Bulega
01/12/2016
BUTINZYA
Kijiji cha Mbula
Mbunge kutembelea shule ya S/M Mbula iliyoezuliwa na mvua iliyoambatana na  upepo
·         Darasa moja kuezuliwa na kudondosha ukuta
·         Mbunge alitoa kiasi cha fedha kwa ajili ya ukarabati wa darasa hilo

Comments