Wakazi wa Uyovu-Bukombe wanyeshewa mvua na Mbunge wao

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisalimiana na viongozi wa Kitongoji cha Azimio Kata ya Uyovu alipowasili hapo kwa ajili ya mkutano wa hadhara



 Diwani wa Kata ya Uyovu Mhe. Usuph Fungameza  na pembeni ni mwanachi wa Kitongoji hicho akimlalamikia Diwani huyo kwa kitendo cha mkukkaribisha mwenyekiti wa kitongoji  hicho kufungua mkutano ambaye wananchi hao walimkataa kupitia mkutano wa hadhara.

 Wananchi wakiwa katika umakini wa kusikiliza Mbunge wao Mhe. Doto Mashaka Biteko.
 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiendeleza mkutano ndani ya mvua  na wananchi wa Kitongoji cha Azimio 


Picha ya wananchi wa kitongoji cha Azimio Kata ya Uyovu  wakionyesha upendo na uhitaji wao juu ya  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa kumsikiliza ndani ya  mvua ikiwa inanyesha.



Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani  Geita,Mhe. Doto Mashaka Biteko
amewataka wananchi wa Kitongoji cha Azimio kilichoko katika Kijiji cha Ibamba hasa  vijana kuachana na  siasa zisizo na tija badala yake  kuanzisha   vikundi mbalimbali vya maendeleo ili kunufaika na serikali yao kwa kujiletea maendeleo yao kwa mtu mmojammoja na kwa  haraka.


Mhe.  Biteko aliyasema hayo kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika katika  Kijiji cha Ibamba  Kata ya Uyovu  alipokwenda kuonana na  wananchi ili kujadiliana shughuli za maendeleo  na kusikiliza kero zao.

Alisema inahitajika nguvu ya pamoja ili kuhakikisha wana maliza changamoto za eneo hilo, zikiwemo ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, kituo cha Afya, miradi ya maji na upungufu wa Shule hali inayowasababishia wanafunzi kusoma darasa moja wakiwa wamebanana sana huku wengine wakisomea nje huku akiitolea mfano shule ya  msingi Ibamba yenye   idadi ya  wanafunzi 1200 kwa darasa la kwanza peke yake .
 
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko alisema yupo tayari kushirikiana na vijana hao katika kujikwamua na wimbi la umaskini huku akiwasihi wajitokeze kwa wingi kwenye eneo lililoonekana na madini katika Pori la Halmashauri ya Bukombe(Kerezia) na kujishughulisha kwa kadri mtu anavyoweza huku akiwasihi watu wenye leseni ya uchimabi wa madini  katika maeneo hayo kulegeza masharti ili watu wenye uwezo wa chini waweze kushiriki kujitafutia riziki katika eneo hilo.


Comments