Waganga wa Tiba Asili Wilayani Bukombe wakutana na Viongozi wa Kiserikali

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Josephat Maganga (aliyevaa miwani) kushoto ni mwenyekiti wa umoja wa waganga wa tiba asili  Wilayani Bukombe(UWAWABU) Bw. Mhamed Hamis na viogozi wengine wa kiserikali nawa jadi wakiwa katika mkutano wa waganga wa tiba asili kwenye ukumbi wa Amani-Ushirombo Mjini.

Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakiwa katika mkutano  wa umoja wa waganga wa tiba asili  Wilayani Bukombe(UWAWABU).
 


Picha ya baadhi ya Waganga wa tiba asili wakiwa katika umakini wa kusikiliza
 


Mmoja wa waganga hao Bw. Nasib Hamad akizungumzia adha na kero zinawakumba katika kazi zao.



Bw. Lubanga Mdima ambae pia ni mganga wa tiba asili iliiomba serikali iwatambue uwepo wao  na kuwasaidia ili wasinyanyasike kupitia viongozi wa serikali wanaojichukulia madaraka mkono bila kujali sheria inasemaje.  



 Bw. Khamis Ngarama nae ni mmoja wa waganga wa tiba asili akizidi akielezea changamoto zinazowakumba waganga hao katika shughuli zao za tiba asili.  



Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko alianza kwa kuwapa pole kwa usunbufu wanaoupata juu ya baadhi  viongozi wa serikali wasio waadilifu na  kuahidi kuwa nao bega kwa bega waganga hao ili kuhakikisha wanakaa kwa amani na kuwasihi wazingatie sheria ili kuendelea kuilinda tunu ya amani ya nchi yetu kwa kutofanya ramli chonganishi pia kutoshiriki kabisa katika mauaji ya vikongwe vilevile ukataji wa viungo vya walemavu wa ngozi(albino).  



Waganga wa tiba asili  Wilayani Bukombe(UWAWABU) wakimsikiliza Mbunge wao Mhe. Doto Mashaka Biteko katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Amani Kata ya Igulwa- Ushirombo Mjini.





Comments