Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (Katikati) akiwasili kwenye Kikao na waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha.
Baadhi ya waendesha boda boda wakifuatilia kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Polycarp Nkuyumba(aliyesimama) akiwakaribisha viongozi na wadau kwenye Kikao na waendesha boda boda wa Wilaya ya Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo (aliyesimama) akiongea na madereva wa boda boda kuwaelezea mpango wa Serikali wa kuwapatia Pikipiki 200.
Lucas Malusu ni dereva wa boda boda Kutoka Kata ya Elerai (aliyesimama katikati) akitoa maoni yake katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Serafini Shirima(aliyesimama) ni dereva wa boda boda kutoka Kata ya Levolosi akichangia uanzishwaji wa umoja wa wandesha boda boda Wilaya ya Arusha (UBOJA)
Viongozi wa mpito waliochanguliwa kusimamia taratibu za uanzishjwaji wa Umoja huo pamoja na utoaji wa Pikipiki wa vijana nane wa Kila Kata.

Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyesimama mbele) akihitimisha kikao
chake na waendesha boda boda wa Wilaya ya Arusha.
Nteghenjwa Hosseah
Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amekutana na waendesha bodaboda
wa Jiji la Arusha na kuwajulisha kuhusu mpango wa Serikali wa
kuwakwamua kiuchumi kwa kuwawezesha kupata Pikipiki bila Riba wala
dhamana.
Rc Gambo
amekuja na Mpango huu wa Kuinua uchumi wa Vijana kwa kuwapatia Pikipiki
baada ya kukutana na kundi hili la waendesha boda boda kwa mara na
kusikiliza malalamiko yao huku miongoni mwa kero yao kubwa ni kutozwa
fedha nyingi na wamiliki wa boda boda hizo.
Akiongea
na waendesha boda boda Rc Gambo alisema ninaona jinsi mnavyojituma
katika kujitafutia riziki lakini hamthaminiki na kazi hii imekua
ikidharaulika, sasa muda umefika kwa kazi hii kuwa ya heshima mbele ya
Jamii, kila kijana aliyepo katika biashara hii ataweza kumiliki
Pikipiki yake na sio kuendesha Pikipiki za watu ambao wamekuwa
wakiwanyonya kila siku kwa kuwatoza Fedha nyingi na wao kuzidi kuneemeka
wakati ninyi mnazidi kuwa masikini.
“Kundi
hili limekuwa likitumiwa kwa maslahi ya watu wachache kwa kuwa wamekuwa
wakipewa Pikipiki hizo kwa faidi kubwa na mmiliki anapokea Fedha zaidi
yya mara mbili ya bei ya kununulia Pikipiki hiyo ndipo aamue
kummilikisha kijana pikipiki hiyo au aamue kuendelea kupokea Fedha kwa
kipindi chote wakati ninyi mnapata tabu barabarani huko na mnaambulia
Fedha kidogo kiasi ambacho hamuwezi fikia hatua ya kumiliki Pikipiki
zenu” Alisema Gambo.
Aliongeza
kuwa Serikali ya Mkoa wa Arusha imeona ni vyema ikawajengea uwezo
vijana waliopo katika kazi hii kwa kuwapa mafunzo na kuwapatia Pikipiki
ambazo mtatakiwa kurejesha kiasi cha Fedha halali iliyonunuliwa Pikipiki
hiyo kisha kumilikishwa chombo bila ya riba yeyote wala dhamana.
Aliendelea
kusema utoaji wa Pikipiki hizi utazingatia Kata zote zilizopo katika
Jiji la Arusha ili Pikipiki ziweze kuwafikia walengwa na zoezi hili
litaendelea kwa vijana wengine kadiri ya mahitaji; Tutaongeza usimamizi
kwa wote watakaopata Pikipiki hizi ili waweze kurejesha Fedha kama
inavyotakiwa na tuweze kuwanunulia vijana wengine hatimaye tuwafikie
vijana wote wenye uhitaji wa kumiliki na kufanya biashara ya bodaboda.
Serafini
Shirima ni dereva wa boda boda Kata ya Levolosi akizungumza katika
Kikao hicho alisema kwa mara ya kwanza Katika Mkoa huu wamepata mlezi
anayetambua na kuthamini kazi ya boda boda na aliyethubutu kuwatafutia
Pikipiki za bei nafuu ili kuongeza kipato cha vijana wa Arusha.
Shirima
alishauri kuundwa kwa kamati ya mpito itakayosimamia na kuratibu
mchakato mzima wa vijana watakaoanza kupewa Pikipiki hizo na kukamilisha
taratibu zote za uanzishaji wa umoja wa wandesha Boda boda
utakaofahamika kwa jina la (UBOJA) chini ya Mlezi Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mhe. Gambo.
RC Gambo
alikamilisha Kikao hicho kwa kusimamia uchaguzi wa viongozi wa mpito
kutoka katika Kila Kata na hatimaye kupatikana viongozi watano
watakaoratibu mpango wa awali wa utoaji wa Pikipiki kwa vijana.
Pikipiki
zitakazotolewa katika awamu ya kwanza ni 200 zikiwa na thamani ya Tsh
Mil 400 na zitatolewa sanjari na Bima kubwa(Comprehensive Insurance) kwa
vijana 200 ambapo kila Kata itatakiwa kutoa vijana 8.
Vijana wa
Arusha watakabidhiwa Pikipiki hizi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa tarehe 03/12/2016 kwenye
uwanja wa Sheikh Amri Abeid.(P.T)
Comments
Post a Comment