Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli amlaki
mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara baada ya
kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli
akimtambulisha na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby
Itno kwa viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama mara baada ya
kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa
na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara baada
ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli
akimzawadia kinyago cha Kimakonde cha "Umoja" na picha ya kuchora ya
tembo na Mlima Kilimanjaro na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe
Idriss Deby Itno mara baada ya kiongozi huyo kuwasili kwa mazungumzo
Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli
akimzawadia kinyago cha Kimakonde cha "Umoja" na picha ya kuchora ya
tembo na Mlima Kilimanjaro na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe
Idriss Deby Itno mara baada ya kiongozi huyo kuwasili kwa mazungumzo
Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno akipokea shada ya maua
mara baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba
27, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akisalimiana na mabalozi
wanaowakilisha nchi mbalimbali za Afrika nchini mara tu baada ya
kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo
Novemba 27, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa
na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu
wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa na mizinga 11 mara baada ya
kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akikagua gwaride rasmi i
mara tu baada ya kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
jioni ya leo Novemba 27, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli
akimtambulisha Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu kwa
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe kassim Majaliwa
baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016.
Rais
wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu leo tarehe 27 Novemba,
2016 majira ya jioni amewasili hapa nchini kwa ziara ya kiserikali ya
siku 3 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Rais Lungu amepokelewa na mwenyeji wake Rais Magufuli na kulakiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hapa nchini pamoja na wananchi.
Akiwa uwanjani hapo Rais Lungu amepokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kesho tarehe 28 Novemba, 2016 Rais Lungu ataendelea na ziara yake hapa nchini ambapo pamoja na kutembelea miradi ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia ikiwemo TAZARA na TAZAMA, atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, atashuhudia utiaji saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia na jioni atahudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Magufuli kwa ajili yake Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe. Idriss Deby Itno leo tarehe 27 Novemba, 2016 majira ya alasiri amewasili hapa nchini kwa ziara kikazi ya siku 2.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Rais Idriss Deby Itno akiwa na Mkewe Mama Hinda Deby amepokelewa na mwenyeji wake Rais Magufuli na kisha kulakiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na wananchi.
Jioni hii, Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Rais Idriss Deby Itno Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Comments
Post a Comment