RAIS MAGUFULI ASAINI MUSWADA WA SHERIA YA VYOMBO VYA HABARI

RAIS John Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016.
Taarifa ya Ikulu jijini Dar es Salaam imesema Rais Magufuli ametia saini sheria hiyo jana ikiwa ni siku 10 baada ya kupitishwa na Bunge la 11 la Tanzania katika Mkutano wake wa 5 Mjini Dodoma.
Aidha Rais amewapongeza wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwa Sheria hiyo.
"Naamini kuwa Sheria hii itasaidia kuboresha sekta ya habari kwa manufaa ya wanataaluma wenyewe na Taifa," alisema Rais Magufuli
 

Comments