MWIGULU AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU UHAMIAJI, ATEMBELEA NYUMBA ZA MAKAMISHNA NA KIWANDA CHA UCHAPISHAJI NYARAKA
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akizungumza na wateja
waliofika kupata huduma katika ofisi za Makao Makuu ya Idara ya
Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Kaimu Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli Mwigulu alifanya ziara katika
idara hiyo kwa kutembelea maeneo ya utendaji katika ofisi hizo,
alizungumza na maafisa na askari Uhamiaji na baadaye alitembelea mradi
wa nyumba za Makamishna na Kiwanda cha Uchapishaji Nyaraka za Uhamiaji,
zilizopo Kijichi jijini humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Kaimu Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (kulia) alipokuwa anatoa hotuba
fupi na baadaye kumkaribisha Waziri huyo kuzungumza na maafisa na askari
wa Uhamiaji wa Makao Makuu wa Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es
Salaam. Katika hotuba yake Waziri Mwigulu aliwataka askari hao waongeze
juhudi zaidi ya kuwakamata wahamiaji haramu na kuwachukulia hatua kali
bila kuwaonea watu katika ukamataji wao. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (aliyevaa tai) na Kaimu
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli wakitoka moja ya nyumba
zinazojengwa kwa ajili ya Makamishna wa Uhamiaji, Kijichi, jijini Dar es
Salaam. Waziri Mwigulu alizikagua nyumba hizo ambazo zipo hatua za
mwisho kukamilika. Waziri huyo alifanya ziara katika idara hiyo kwa
kutembelea maeneo ya utendaji katika ofisi hizo na baadaye alitembelea
mradi wa nyumba za Makamishna na Kiwanda cha Uchapishaji Nyaraka za
Uhamiaji, zilizopo Kijichi jijini humo. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (aliyevaa tai) akiangalia fomu
za kuomba pasipoti za Idara ya Uhamiaji mara baada ya kuchapishwa katika
kiwanda hicho kilichopo Kijichi, jijini Dar es Salaam. Waziri Mwigulu
alikitembelea kiwanda hicho pamoja na Mradi wa nyumba za Makamishna
zinazojengwa katika eneo hilo. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji, Victoria Lembeli. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na Makamishna,
Maafisa na Askari wa Uhamiaji katika ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo,
Kurasini jijini Dar es Salaam. Mwigulu aliwaambia aliwapongeza
watumishi hao kwa kazi nzuri wanayoifanya na aliwataka waongeze juhudi
zaidi ya kuwakamata wahamiaji haramu na kuwachukulia hatua kali bila
kuwaonea watu katika ukamataji wao. Waziri huyo alifanya ziara katika
idara hiyo kwa kutembelea maeneo ya utendaji katika ofisi hizo na
baadaye alitembelea mradi wa nyumba za Makamishna na Kiwanda cha
Uchapishaji Nyaraka za Uhamiaji, zilizopo Kijichi jijini humo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (aliyevaa tai) akikaribishwa na
Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli (kulia)
pamoja na maafisa waandamizi wa Idara hiyo katika ofisi za Makao Makuu,
Kurasini jijini Dar es Salaam. Mwigulu alifanya ziara katika idara hiyo
kwa kutembelea maeneo ya utendaji katika ofisi hizo, alizungumza na
maafisa na askari Uhamiaji na baadaye alitembelea mradi wa nyumba za
Makamishna na Kiwanda cha Uchapishaji Nyaraka za Uhamiaji, zilizopo
Kijichi jijini humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Comments
Post a Comment