Mhe Doto atoa misaada na faraja kwa wahanga wa mvua katika Kijiji cha Namonge

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko, Baadhi ya Waheshimiwa Madiwa na Kamati ya maafa ya Wilaya ya Bukombe kwa pamoja wakiangalia jinsi Shule ya msingi Namonge ilivyoharibiwa vibaya na mvua iliyoambatana na upepo Novemba7/2016 .
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akitoa msaada wa pesa Taslimu laki tano kwa ajili ya ukarabati wa nyumba iliyoezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo kwa mama mjane Bi Rehema Juma miaka 60 mwenye wajukuu watatu na kati ya wajukuu hao mmoja ni mlemavu.


Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assembles of God (TAG) lililoko katika Kijiji cha Namonge Rev. Jacob Ernest akihesabu fedha za ukurabati wa Kanisa zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko baada ya kanisa hilo kuezuliwa na mvua ya upepo.
Hali halisi ya Kanisa la Tanzania Assembles of God (TAG) lililoko katika Kijiji cha Namonge baada mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali. 

Mmoja wa wahanga hao Bi Malta Petro miaka 72 akimshukuru kwa dhati na kumkumbatia Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko baada ya kupewa fedha za ukarabati wa nyumba yake iliyoezuliwa na mvua ya upepo upande mmoja.

Comments