Mhe. Doto ajiridhisha na matengenezo ya barabara ya Uyovu-Kabagole

  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na mhandisi wa ujenzi wa Barabara wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Eng. Chacha M. Moseti kwa makini wakiangalia kina cha Daraja lililoko Kabagole ikiwa ni hatua ya kujiridhisha kwa kukagua mapungufu ya matengenezo ya barabara hiyo ya Uyovu, Kabagole-Nakayenze.



   Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akimpongeza Mhandisi wa ujenzi wa Barabara wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Eng. Chacha M. Moseti kwa usimamizi wake mzuri wa barabara hiyo ya Uyovu, Kabagole hadi Nakayenze yenye urefu wa kilomita kumi na saba iliyofadhiliwa na Shirika la MIVAF kwa gharama ya shilingi milioni 720.

Mhe. Doto alisema  lengo la barabara hiyo ni kuwawezesha wakulima wa maeneo hayo kulifikia soko la mazao kwa urahisi zaidi hasa zao la udaga na kuwasihi wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama pale wanapomuona mtu akiharibu barabara hiyo kwa makusudi.


Comments