MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AONGOZA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KATIKA MAPOKEZI YA MWILI WA SPIKA MSTAAFU MHE. SAMUEL SITTA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimpokea mjane wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania
na
Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta, Mama Margaret Sitta
(kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Jeneza
lenye mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta likiwa
limebebwa na askari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwaongoza viongozi mbali mbali wakati wa mapokezi ya mwili wa Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi
Mstafu Marehemu Samuel Sitta

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
pamoja na Katibu Mkuu wa UWT Mhe. Amina Makilagi (kushoto) wakimfariji
akimfariji Mama Margaret Sitta (katikati) wakati wa mapokezi ya mwili wa
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri
Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta kwenye uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

...............................................
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
ameongoza viongozi na wananchi katika mapokezi ya Mwili wa Spika Mstaafu
Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam ukitokea nchini Ujerumani alipofariki
wakati anapatiwa matibabu.
Akizungumzia
jinsi anavyomfahamu Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Taifa
limeondokewa kiongozi mwadilifu,mzalendo, mchapakazi na mtetezi wa
wanyonge hivyo taifa litaendelea kuumuenzi utendaji wake.
Viongozi
mbalimbali waliojumuika na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan katika mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu
Samweli Sitta kweye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere ni
pamoja na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Seif Ali
Iddi, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika, Kikanda na
Kimataifa Dkt Augustine Mahiga na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda.
Baada
ya Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta kuwasili nchini leo mchana
amepelekwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam ambapo hapo kesho
asubuhi viongozi na wananchi watatoa heshima zao ya mwisho za kuuaga
mwili wa marehemu katika viwanja wa Karimjee jijini
Comments
Post a Comment