Lowasa atinga Bungeni

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa leo (Jumanne) ametinga bungeni kwa ajili ya kuhudhuria shughuli za Bunge la 11, linaloendelea mjini humo.

Lowasa ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM amewasili katika viwanja vya Bumge leo saa 2:38 asubuhi.

Baada ya kuwasili uwanjani hapo alisalimiana na baadhi ya wabunge wa kambi rasmi ya upinzani na wa CCM.

Comments