Lipumba-Sina tatizo na Wazanzibari

                                                                                                                                                                                      MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba amesema hana tatizo na
wananchi wa Zanzibar na kusisitiza kuwa, suala la Muungano ni la muhimu kwa ulinzi na usalama wa Taifa.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho katika kikao cha ndani kilichojumuisha wawakilishi kutoka katika wilaya sita za Ushetu, Geita, Mbogwe, Sengerema, Kahama pamoja na Kibondo.
Lipumba amesema, kwa sasa yeye na wafuasi wake wamejipanga kukijenga chama hicho na kuongeza kuwa katika kipindi cha nyuma amekuwa mstari wa mbele katika kuwatetea Wazanzibari katika kupata haki zao.
Katika kikao hicho pia Mwenyekiti huyo wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahimu Lipumba hakusita kumsifu aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge la Tisa, Samuel Sitta aliyefariki dunia hivi karibuni kwa kutoa fursa nyingi za kuuliza maswali bungeni kwa kambi za upinzani.
Amesema kuwa baadhi ya wabunge wengi walijengewa uwezo na Sitta katika kuuliza maswali mbalimbali ambayo yalikuwa na maslahi ya nchi na kuongeza kuwa hawatamsahau Sitta katika mchango wake huo.
Kuhusu Katibu Mkuu wa chama hicho, Seif Sharif Hamad, Profesa Lipumba alisema kuwa kama katibu huyo hamtambui yeye kuwa ni Mwenyekiti wake, basi yupo tayari kuzuia mikutano yake yote ambayo angeweza kuifanya Tanzania Bara wakati huu.

Comments