Hillary Clinton amelaumu shirika la FBI kwa kushindwa kwake
Aliyekuwa
mgombea wa kiti cha urais wa Marekani kwa tikiti ya Chama cha
Democratic Hillary Clinton, amesema kwamba kushindwa kwake ghafla katika
uchaguzi uliyopita, kulichangiwa pakubwa na hatua ya mkurugenzi wa
shirika la kijesusi la Marekani FBI, James Comey kutangaza uchunguzi
mpya wa sakata ya barua pepe dhidi yake muda mfupi kabla ya uchaguzi.
Bi
Clinton amewaambia wafadhili wa chama chake kwamba hatua ya Comey
ilisambaratisha kampeini yake, licha ya uchunguzi huo kutompata na
hatia.
Mwandishi
wa BBC nchini Marekani hata hivyo amesema wengi wanahisi kuna msururu
wa sababu zilizomfanya Donald Trump kumshinda katika uchaguzi huo.
Maelfu ya waandamanaji walifanya maandamano kwa siku nne mfululizo dhidi ya rais mteule Donald Trump
Mkurugenzi mkuu wa shirika la kijasusi nchini Marekani FBI James Comey
Mjini New York ,maafisa wa polisi waliwazuia waandamanaji waliojaribu kukaribia bustani ya Union Square.
Wengine walielekea katika jumba la Trump Tower,nyumbani kwa bwana Trump pamoja na makao makuu ya biashara za Trump. BBC
Comments
Post a Comment