Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Ushirikiano
wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na China katika nyanja mbalimbali
zikiwemo za Sanaa na Utamaduni umekuwa chachu kubwa katika kuwajengea
uwezo wasanii wetu na kutekeleza shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na
wataalamu kutoka pande hizi mbili.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye alipokua akizindua wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China
katika Ukumbi wa Utamaduni wa watu wa China leo jijini Dar es Salaam.
“Kwa
miaka mingi Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano uliotoa fursa kwa
watu wake kujifunza shughuli za sanaa na kiutamaduni zilizoko katika
kila nchi hivyo kuendeleza na kuuenzi ushirikiano uliopo katika sekta za
Sanaa na Stamaduni” amesema Mhe. Nnauye
Mhe.
Nnauye amesema kuwa ushirikiano wa nchi hizi mbili umeweza kukua,
kuboresha na kuendeleza wasanii wetu hasa katika kipindi hiki cha
maonyesho ambapo hutoa nafasi kwa wasanii wa Tanzania kujifunza mambo
mbalimbali ya kiutamaduni na kuwapa wasanii wa hapa nchini fursa ya
kufanya maonyesho kama haya nchini China.
Kwa
upande wake Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong
amesema kuwa Maonyesho ya Utamaduni wa China hapa nchini yanatoa fursa
nzuri kwa wananchi wa Tanzania kuelewa na kujifunza utamaduni na sanaa
ya China, kuimarisha ushirikiano wa utamaduni wa China na Tanzania
pamoja na kukuza urafiki wan chi hizi mbili.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen
Hongmin amesema kuwa China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika
kubadilishana uzoefu kwa sekta ya Sanaa na Utamaduni na kujifunza mambo
mapya ili kuendeleza Utamaduni, ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia
kati ya nchi hizi mbili.
Wiki
ya Maonyesho ya Utamaduni wa China itakuwa na maonyesho mbalimbali kama
vile maonyesho ya sarakasi ya Kichina, maonyesho ya picha, hadhara za
opera za China, Udaktari wa kijadi wa China na Utamaduni wa mazoezi
maalumu yanayojenga afya yaitwayo Qigong.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto)
akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa
Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. (katikati
mbele) ni Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong.
Kaimu
Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (kulia) akiteta jambo
na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
alipokua akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa
uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei.

Mkuu
wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei akizungumza na
washiriki wa maonyesho (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho
ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong akizungumza na
washiriki wa maonyesho (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho
ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
akizungumza na washiriki wa maonyesho (hawapo pichani) wakati wa
uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi
ya washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni wa China wakifuatilia
kwa makini matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi
wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto
waliokaa ni Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong
Kikundi
cha Utamaduni na Sanaa cha Jiangxi kikionyesha sarakasi wakati wa
uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
Msanii
kutoka China akionyesha mchezo wa utamaduni wa mazoezi maalumu
yanayojenga afya yaitwayo Qigong wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya
Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
(katikati) katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa China nchini
Tanzania Bw. GOU Haodong (wapili kulia) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho
ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kituo
cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei na wapili kushoto ni
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen
Hongmin

Washiriki
wa Maonyesho ya wiki ya Utamaduni wa China kutoka Chama cha Mchezo wa
WUSHU Tanzania katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya
Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
(katikati) akimsikiliza Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU
Haodong (kulia) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China
leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin.
Comments
Post a Comment