Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January
Makamba akiangalia eneo lililokuwa likitumiwa na Jema Sitalike Project
ambao walizuiwa kuendelea na shughuli za uchenjuaji wa dhahabu kutokana
na kutokuwa na vibali. Wengine katika picha ni pamoja Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga.
Mashimo
yaliyokuwa yakitumiwa na Jema Sitalike Project ambao walizuiwa
kuendelea na shughuli za uchenjuaji wa dhahabu kutokana na kutokuwa na
vibali, yakiwa yameachwa wazi hali inayotishia usalama wa wananchi
wanaozuka maeneo hayo. Waziri Makamba ameagiza kusimamishwa kwa shughuli
za Mradi wa Jema ambao kwa sasa wamehamishia shughuli zao Mkoani Mwanza
na kuwataka kuchukua hatua za haraka kufunika mashimo yaliyopo Sitalike
- Katavi.
Na Lulu Mussa, Katavi
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba amesema kuwa uharibifu wa Mazingira katika Mto Katuma ni tishio
kubwa kwa uhai wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi na wakazi wa Mkoa huo.
Akiwa
katika mwendelezo wa ziara yake ya siku 16 kutembelea Mikoa mbalimbali
hapa nchini, Waziri Makamba amesema kuwa Mto Kasuma uko hatarini
kutoweka kutokana na ongezeko la shughuli za binadamu, wingi wa mifugo,
Uchimbaji wa madini, ukataji wa miti na uchepushaji wa maji
kunakopelekea kupoteza mtiririko wa maji yenyewe.
Waziri
Makamba amesema ni vema kuwa na mikakati na hatua za haraka na zile za
muda mrefu ikiwa ni pamoja na kufanya sensa ya mifugo ili kuweza kujua
Mkoa una mifugo kiasi gani na kuainisha maeneo ya malisho. "Zoezi hili
si hiari, ni lazima na takwa la kisheria' Makamba alisisitiza.
Imependekezwa
pia kufanyika kwa Ubomoaji wa mabanio yanayokinga maji kama hatua ya
haraka ili maji yaweze kutiririka kwa wingi katika kipindi hiki cha
kiangazi, na kuagiza kufanyika kwa doria za mara kwa mara ili kubaini
watu wanaokiuka taratibu hizo.
Waziri
Makamba pia amezitaka Mamlaka za bonde kutimiza wajibu wao kwa kutoa
vibali stahiki kulingana na ujazo wa maji uliopo katika maeneo yao ili
kujenga usawa wa matumizi sahihi ya rasilimali maji. ' Mamlaka za bonde
zisitoe vibali ofisini na operesheni ifanyike kwa wote wasio na vibali"
Alisema Waziri Makamba.
Pia,
Waziri Makamba ameagiza kufanyika kwa Tathimini ya athari kwa mazingira
kwa Mto Kasuma na kuuagiza uongozi wa Mkoa wa Katavi kuainisha baadhi
ya maeneo ambayo yatatangazwa kama maeneo nyeti ili kunusuru mazingira
ya Katavi na ustawi wa Mto Katuma.
"Kuwe na tozo ya uharibifu wa Mazingira na tozo hiyo iendane na kiwango cha uharibifu atakachofonya muhusika" ,Akiongea
na Wadau wa Mazingira katika Ukumbi wa Maji Mkoani Katavi Waziri
Makamba amekumbusha watumishi wa Umma Nchini kuwa na nidhamu na
uwajibikaji wa dhati na kusisitiza kuwa hakuna muda wa kubembelezana.
"Fanyeni kazi kwa weledi, nidhamu na uadilifu" alisema Makamba.
Katika
hatua nyingine Waziri Makamba ametembelea eneo ulipokuwa mradi wa
uchenjuaji wa dhahabu wa Jema Sitalike Project ambao ulikua ukifanya
shughuli zake bila kibali cha Wizara ya Nishati na Madini na Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Waziri
Makamba ameagiza kusimamishwa kwa shughuli za Mradi wa Jema ambao kwa
sasa wamehamishia shughuli zao Mkoani Mwanza na kuwataka kuchukua hatua
za haraka kufunika mashimo yaliyopo Sitalike - Katavi ili kunusuru uhai
wa viumbe vinavyozunguka maeneo ya Sitalike.
Waziri
Makamba yuko Mkoani Katavi kwa ziara ya kikazi na hii leo amekutana na
Viongozi wa Vikundi vya Mazingira, katembelea eneo lilikokuwa na
shughuli za Uchimbaji wa Madini na chanzo cha Mto Katuma.
Comments
Post a Comment