Wakazi wa Mji Mwema-Namonge huko Bukombe Wamlaki Mbunge wao.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisalimiana na Diwani wa Kata ya Namonge Mhe. Mlalu Bundala alipowasili katika Kijiji cha Mji Mwema kwa ajili ya kuongea na wakazi wa Kijiji hicho.

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akilakiwa na kupokelewa kwa shangwe kubwa sana na wakazi wa Kijiji cha Mji Mwema kilichoko Kata ya Namonge.

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mji Mwema na viunga vyake na kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mwakilishi wao na kuwaahidi kufanya kazi hiyo kwa nguvu zake zote.

Wakati akizungumza na wakazi hao alisema vijiji vyote Hamsini na mbili vya Wilaya ya Bukombe vitapata Umeme kupitia mradi wa umeme vijijini (REA) na Vijiji kumi kupata Mradi wa Maji ikiwa ni hatua madhubuti ya serikali kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Bukombe wanapata maendeleo kwa haraka na huduma nzuri.

Pia aliwasihi wananchi hao kufanya kazi kwa bidii na kwa umoja bila kujali dini,ukabila wala aina za vyama ili kujiletea maendeleo huku akiahidi kuwatetea wanyonge kwa nguvu zake zote bila kujali itikadi zao. 

 Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Mji Mwema wakimsikiliza Mbunge wao Mhe. Doto Mashaka Biteko katika Mkutano uliyofanyika kwenye Kijiji cha Mji Mwema Kata ya Namonge.
 Picha ya baadhi ya Wananchi waliyouliza maswali kwenye mkutano huo ikwa ni pamoja na kuorodhesha changamoto zao ambazo ni ucheleweshwaji wa pembejeo, huku wakilalamikia ukosefu wa miundo mbinu ya barabara hali inayowasababishia  wakulima hao kutokufikisha mazao yao sokoni kwa wakati na kuwasababishia uchumi wa kuyumba sana.

Comments