Mbunge wa Bukombe atoa chakula kwa watahiniwa wa Kidato cha nne Ushirombo Sekondari

 Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilayani Bukombe Bi. Twaiba Musa Mkangala akisaini katika kitabu cha wageni alipowasili Shule ya Sekondari Ushirombo kwa ajili ya kukabidhi Chakula cha watahiniwa wa kidato cha nne kilichotolewa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.

 Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilayani Bukombe Bi. Twaiba Musa Mkangala akimkabidhi barua  Mkuu wa Shule ya Sekondari Ushirombo Mwl Juma Luguha iliyotoka kwa  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.

  Mkuu wa Shule ya Sekondari Ushirombo Mwl Juma Luguha akiwasomea barua wanafunzi wa kidato cha nne  iliyotoka kwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko   yenye Ujumbe wa kuwatakia heri ya Mtihani wa kumaliza kidato cha nne.Nayo ni 



 Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne wakisikiliza kwa makini.


  Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilayani Bukombe Bi. Twaiba Musa Mkangala akizungumza na wanafunzi hao amesema chakula hicho kimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko ambacho ni maharage kg 500,unga wa mahindi kg 780 na mchele  kg 390 vilivyogharimu jumla ya Tsh. 2028,500 ikiwa ni hatua ya kuwaunga mkono na kuwahamasisha kufanya vizuri kitaalama kwa kujisomea kwa pamoja katika kipindi hiki cha mitihani, nakuwasihi wajitahidi wafanye vizuri katika mitihani yao ili kuinusuru shule na Taifa kwa ujumla.
 
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ushirombo wakishughulika na upakuaji wa chakula ikiwa ni hatua ya kuonyesha furaha yao. 



Mmoja wa wanafunzi hao akitoa Shukrani za dhati kwa niaba ya wanafunzi wenzake na kuwahamasisha kufanya vizuri katika mitihani yao ili kutomvunja moyo Mbunge wao Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa alichokifanya.

Comments