RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA HOSTELI ZA WANAFUNZI KATIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe
kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi watatu kutoka (kulia),
Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce
Ndalichako wanne kutoka (kulia) watatu kutoka kushoto, Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa
Rwekaza Mukandara wanne kutoka (kushoto), Mtendaji mkuu wa Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga wakwanza (kulia) Pamoja na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga wakwanza
kushoto.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la
msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Elimu, Sayansi
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara.
Hosteli hizo zitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 3840 na
ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa
mwaka huu.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa hosteli za wanafunzi
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana
jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza
Mukandara mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hosteli
hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA Arch. Elius Mwakalinga akitoa
ufafanuzi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa Hosteli
hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga tumba
katika bendi ya Msondo Ngoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika
mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es
Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mke
wake Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo
ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara wakipiga makofi wakati brass
bendi ya JKT ilipokuwa ikitumbuiza mara baada ya kukamilika kwa tukio
la kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi
katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono
wakati akiwasili katika viwanja vya hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam.
Taaswira
ya moja ya moja ya hosteli hizo za wanafunzi ambazo ujenzi wake umefikia
asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.PICHA NA
IKULU.
Comments
Post a Comment