Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mshaka Biteko akisaini kitabu cha wageni tayari kwa kuaanza mkutano
Mmoja ya Kikundi kilichotoa Burudani(Waswezi)
Picha ya Wanakwaya wa Kikundi cha Hamasa wakitoa Burudani katika mkutano wa Mbunge
Picha ya msanii machachari wa Kijiji cha Kakoyoyo aliyeimba wimbo wenye ujumbe wa kuomba daraja.
Diwani wa Kata ya Bulega akisema na wakazi wa kijiji cha Kakoyoyo
Wananchi wakisikiliza kwa makini Mbunge wao
Wananchi wa Kijiji cha Kakoyoyo, Kata ya
Bulega , Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamemuomba Mbunge wa Jimbo la Bikombe
Mhe. Doto Mashaka Biteko kushirikiana na wafugaji kwa kuihimiza serikali
kuwatengea maeneo ya malisho hasa nyakati za kilimo zinapoanza.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti baadhi ya Wananchi hao Bw Magesa Malima na Malingumu Juma wamesema
kuwa wananchi katika Wilaya hiyo wamekuwa wakihangaika sana
kutafuta maeneo ya malisho hali inayowakwamisha
katika upatikanaji wa maeneo ya maji na chakula cha mifugo yao pa kudumu hivyo
kuwasababisha uchumi wao kuzorota sana.
Katika hatua nyingine Bw Malingumu
Juma amemuomba Doto Mashaka Biteko(Mb) kutoa ushirikiano kwa wananchi kwa
kuisukuma serikali katika swala zima la huduma ya maji ya uhakika katika Kijiji
cha Kakoyoyo pamoja na vijiji jirani ndani ya Kata hiyo ya Bulega,kusaidia
ajira kwa vijana,upungufu wa walimu wa Shule za Kakoyoyo na kumsihi Mbunge huyo
aisukume halmashauri ili iwaletee huduma ya mabarabara ya mitaa kwani wao wako
katika halmashauri ya mji mdogo.
Aidha Mbunbe wa jimbo la
Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko amesema atahakikisha anatoa ushirikiano wa
kutosha kwa wananchi hao hasa katika maswala ya kuiweka Wilaya kuwa na miundo
mbinu ya mabarabara mizuri na kuwaeleza mikakati inayo endelea dhidi ya
barabara zao ikiwemo kuzipandisha hadhi
kutoka barabara zinazohudumiwa na mfuko wa halmashauri hadi kuwa barabara
zinazohudumiwa na wakala wa Barabara Mkoa (Tanroads) na huwasihi wananchi
kufuga kisasa kwa kupunguza idadi ya mifugo ili kupunguza adha zianazo jitokeza
wakati huu ambao serikali ikipitia maeneo yake upya kipita Wizara zenye
dhamana.
Comments
Post a Comment