Wilaya ya
Meatu imeanzisha Kiwanda cha Kusindika Maziwa, huku Maswa ikianzisha
Kiwanda cha Uzalishaji Chaki vyote vikishirikisha makundi ya vijana.
Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema Bariadi inatarajiwa kuanzisha kiwanda
cha kutengeneza sabuni; Busega kitajengwa kiwanda cha maji wakati
mipango zaidi ikiendelea kuangalia kiwanda kinachofaa wilayani Itilima.
Mtaka
alisema katika kutekeleza azma ya Tanzania ya viwanda, mkoa umekuwa
ukifanya jitihada za kuwaunganisha vijana kwa kuwajengea uwezo wa
kujitegemea.
“Ni fedheha
kuona hata bandeji za hospitalini zinatoka nje huku malighafi zake
inapatikana nchini. Ni vyema kuzitumia fursa zilizopo na mikakati ya
kuanzisha kiwanda cha bandeji na maji,” alisema Mtaka.
Katika kutekeleza kaulimbiu ya mkoa huo ya ‘One district one product’, wanatarajia kuwashirikisha vijana na kuwajengea uwezo ili wafanye kazi za kujiletea maendeleo.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye
Ulemavu), Jenista Mhagama alisema wizara yake itaendelea kuwaunga mkono
vijana wanaothubutu kwa kuwapa mikopo ili waazishe miradi.
Mhagama
alisema vijana wa Simiyu wameonyesha njia kwa wenzao nchini na
kuwaahidi kuwapa mkopo wa Sh30 kwa kuanzisha kiwanda cha chaki na
maziwa.
Aliwataka vijana kuchangamkia fursa badala ya kukaa vijiweni na kulalamika kuwa hawana kazi.
Comments
Post a Comment