Mhe.Doto achota baraka kwa watumishi wa Mungu Siloka





 Mwenyekiti wa Umoja  wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) Tarafa ya Siloka Mchungaji Sylvanus Fakumuha akifungua Mkutano.

 Mchungaji Jonathan Kasase akifungua mkutano kwa maombi
Viongozi wa Umoja  wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko wakishiriki katika maombi





Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na Wachungaji wa Umoja  wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) Tarafa ya Siloka.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akijichotea baraka kwa kuwanawisha watumishi wa Mungu.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko  akiwa na viongozi wa Umoja  wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) Tarafa ya Siloka. 

 Picha ya Pamoja baada ya mkutano.





Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita Mhe,Doto Mashaka Biteko amekutana na wachungaji wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste(CPCT) wa Tarafa ya Siloka na kufanya mazungumzo nao sambamba na kutoa shukrani za dhati kwa uhamasishaji wao kwenye ushindi wake na kuwaahidi kutenda haki ya kusimamia ukweli tu na kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupeleka mawazo yao hivyo wamuunge mkono kwa kumuombea.

Aidha katika mkutano huo Wachungaji waliorodhesha changamoto zao ikiwa ni pamoja na miundo mbinu duni ya barabara,ukosefu wa kituo cha afya sambasamba na dawa na mifuko ya kutunzia damu hali inayosabaisha vifo visivyo vya lazima kwa waumini wao, kucheleweshewa pembejeo za kilimo hali inayowakwamisha katika uzalishaji  bidhaa zinazotokana na kilimo cha mazao na kusababisha uchumi wao kuyumba. 

 Aidha Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Biteko amewaomba Wachungaji hao  wajitahidi kuwasaidi vijana kuwa na hofu ya Mungu na kufanya kazi kwa bidii ili kulinusuru taifa na kwasihi waumini wao na jamii inayowazunguka kwa ujumla kufanya kazi kwa kila mtu katika eneo lake ili kuharakisha maendeleo.
 






Comments