Meza kuu tayari kwa Sherehe
Wageni waalikwa wakiwa katika nafasi zao
Mmoja wa walimu katika maadhimisho hayo akichambua uzuri na changamoto za ualimu.
Hawa ni walimu wakiwa wamepita mbele katika madhimisho hayo kwa ajili ya kutoa Burudani wakiongozwa na Mama Mstaafu ambae jina lake halikuweza kutambulika kwa haraka .
Huyu ndiye mshindi wa kwanza akipewa zawadi ya fedha na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambae kwa siku hiyo alikuwa mgeni maalum na kuandaa mpambano huo wa Burudani ya Kucheza.
Picha ya Pamoja ya walimu aliokuwa akifundisha nao katika shule ya msingi Ibamba kabla hajastaafu.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza wakati akitoa zawadi kwa mstaafu Mwl Anathory Kubi
Leo(jana) ikiwa ni siku ya walimu
duniani,Walimu wa Kata ya Uyovu Tarafa ya Siloka Wilaya Bukombe Mkoani Geita
wameungana Walimu Duniani katika maadhimisho
ya mwaka huu yameangukia ndani ya ajenda ya maendeleo endelevu ya
2030(SDG’s) iliyoafikiwa mwaka mmoja uliopita..
Maudhui ya mwaka huu ni “Thamini
Walimu, Boresha Hali zao”, yanajumuisha kanuni za msingi kuhusu ustawi wa
walimu zilizopitishwa miaka 50 iliyopita kwa ushirikiano baina ya UNESCO na
Shirika la Kazi Duniani(ILO), na pia yanamulika lengo nambari nne katika ajenda
ya maendeleo ya “Kuhakikisha elimu bora, shirikishi na yenye usawa na
inayojenga fursa ya maisha ya kujifunza kwa wote”.
Akizungumza
katika maadhimisho hayo yaliyojumuishwa
na kumwaga mstaafu Mwalimu Anathory Kubi,
Mwalimu Doto Mashaka Biteko ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe amesema ni siku
ya furaha sana kwa walimu maana huinua hali ya kufanya kazi na huwavutia watoto
wengi kuipenda kazi ya ualimu na kuwa sisitiza waalimu kuhakikisha kutohawajihusishi
na vitendo vya ulevi, rushwa na hata kuwa na mahausiano ya mapenzi na wanafunzi
mambo haya yanapotendeka yanatupunguzia hadhi kwa jamii na kujenga taifa lisilo
na nidham pia aliwataki walimu wenzake
siku njema ya mwalimu duniani.
Kwa upande wake Mwalimu mstaafu
Anatory Kubi amesema kuwa ni muhimu Walimu
washirikiane kwa kila namna kumwondoa
adui yetu mkubwa ujinga, maradhi na magonjwa. Na kuongeza kuwa maadui wote hawa huondolewa kwa urahisi na
Elimu ambayo sisi ndo tunaoitoa kwa watoto wa Taifa letu.
Comments
Post a Comment