Mbunge Doto akutana na Wananchi wa Bukombe Kuinusuru Misitu ya Hifadhi

Hali halisi ya  msitu wa hifadhi wa Kahama-Biharamulo maarufu Pembe la Ng'ombe
 

 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Busonzo pamoja na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ambae pia ni Diwani wa Kata hiyo ya Busonzo Mhe Safari Nikas Mayala  wakimwelezea Mbunge wa Jimbo la Bukombe  Mhe. Doto Mashaka Biteko hali ya wananchi baada ya zoezi la hamahama kupisha eneo la Hifadhi linaloendelea katika Wilaya za jirani . 



  Mbunge wa Jimbo la Bukombe  Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Nampalahara Kata ya Busonzo nakuwaeleza wawe na aman na kuwasihi wasiingie katika Mapori ya Hifadhi na waione misitu hiyo ni hazina  na pia ni wajibu wao kushirikiana na Serikali kuilinda kwa kutojihusisha na ukataji wa miti hovyo.

  Mbunge wa Jimbo la Bukombe  Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwasikiliza wananchi wa Kata ya Busonzo wakimweleza nao hatua wanazozichukua dhidi ya uhifadhi ili kuhakikisha Misitu hiyo ya Hifadhi inaendelea kuwepo vizazi hadi vizazi


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ambae pia ni Diwani wa Kata hiyo ya Busonzo Mhe Safari Nikas Mayala akizunguza na wakazi hao wa Kijiji cha Nampalahara huku wakiwa na nyuso za furaha.

Comments