Mbunge Doto akutana na wakazi wa Kata ya Bugerenga na kupata kero zao

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisalimiana na kuwasikiliza wazee wa Kijiji cha Bufanka Kata ya Bugerenga mara alipowasili kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi.

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisaini kitabu cha wageni tayari kwa kuanza Mkutano wa hadhara.

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Bufanka Bw. Pastory Salenge akisoma risala kwa niaba ya Mtendaji wa Kata ya Bugerenga.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akihutubia Mkutano wa Hadhara katika Kijiji cha Bufanka Kata ya Bugerenga.



Picha ya Baadhi ya Wananchi walio hudhuria katika mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko uliyofanyika Kijiji cha Bufanka katika Kata ya Bugerenga.





 Picha ya baadhi wananchi waliojitokeka kuuliza maswali katika Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.


 Hali halisi Zahanati ya Kijiji cha Bufanka iliyoanza kujengwa tangu mwaka 1996.
 
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita Mhe,Doto Mashaka Biteko amefanya ziara katika Kijiji cha Bufanka, Kata ya Begerenga, Tarafa ya Bukombe Wilayani Bukombe na kufanya mkutano wa hadhara katika Kijiji hicho ikiwa ni hatua ya kukusanya maoni kutoka kwa wananchi na kuyawasilisha Bungeni.
Katika mkutano huo Mhe, Doto Biteko(Mb) alianza kwa kuwaeleza mikakakati mipango na mambo ambayo yanafanywa na serikali ikiwa ni pamoja kuzipandisha barabara kutoka upande wa halmashauri kuwa barabara zinahudumiwa na mfuko wa mkoa(Tanroad) ili kuboresha miundo mbinu ya barabara katika Kata hiyo na Jimbo zima kwa ujumla.
Aidha katika mkutano huo wananchi waliorodhesha changamoto zao ikiwa ni miundo mbinu duni ya barabara,ukosefu wa kituo cha afya kwa muda mrefu,ukosefu wa malisho ya mifugo yao  na kukosa kabisa huduma ya maji hali inayo wasababishia hata vifo kwa watoto mara wanapokuwa wanakwenda kwenye visima vilivyo wazi na wakati mwingine inakuwa ni usiku hasa wakati wa kiangazi pia kutoona mwendelezo wa Mradi wao wa kilimo cha umwagiliaji Bugerenga hali inayo wavunja moyo wananchi hao kuendelea na kilimo hicho.
Pia Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Biteko amewasihi wananchi wajitahidi kufanya kazi kwa juhudi ili kujiletea maendeleo kwa mtu mmojammoja wakati serikali ikiweka miundo mbinu vizuri na kuwaomba kuzidi kushirikiana kwa pamoja bila kujali itikadi dini wala ukabila  ili kulifikisha taifa  mbali zaidi kwenye upande wa maendeleo na kutoa Shilingi laki moja na themanini kwa ajili ya ujenzi wa choo katika shule ya msingi Bufanka wakati wa mkutano huo.

 

Comments