Katibu Mkuu Wizara ya Maji na
Mwagiliaji, Mbogo Mfutakamba
akibadilishana hati na
Mwakilishi wa Shirika la Afya Dunia
(WHO) Dk. Richard Banda,
Dar es salaam, leo.
|
Na Sheila Simba, Maelezo
Serikali
kupitia Wizara ya Maji na Umwangiliaji, imepokea mchango wa dawa za
kutibu maji aina ya (calcium hypochlorite) kiasi cha kilogramu 49,500
kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zitakazo sambazwa kwa mamlaka
ndogo za maji nchini.
Akipokea
dawa hizo leo Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia
Mbogo Mfutakamba, alisema kuwa dawa hizo zitasambazwa kwenye Halmashauri
mbalimbali kama mchango wa shirika hilo katika kuhakikisha upatikanaji
wa maji safi na salama.
“Naziagiza
Halmashauri na Mamlaka za maji kote nchini ambazo zimeainishwa kupatiwa
dwa hizo kuzitumia kwa usahihi ili kukidhi lengo lililokusudiwa”alisema
Ameeleza
kuwa serikali imejiwekea malengo ifikapo mwaka 2020 kuhakikisha
asilimia 85 wananchi wanaoishi vijijini wanapata majisafi na salama na
asilimia 90 ya wananchi waishio mijini wanapata huduma hiyo muhimu.
Amesema
kuwa dawa hizo zitasambazwa kutokana na uhitaji wa maji katika eneo
husika na kutoa mfano wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga ambayo imepata
mapipa sitini kutokana na kuzalisha maji mengi.
“Serikali
itaendelea kuchangia katika mamlaka za maji ili kuwapatia watu majisafi
ili kuondoka na tatizo la kipindupindu katika baadhi ya maeneo”alisema
Mfutakamba
Akitoa
shukurani kwa niaba ya Serikali ya Tanzania Katibu Mkuu huyo Injia
Mfutakamba,amesema kuwa WHO ni shirika la mfano wa kuigwa na wadau
wengine kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwapitia wananchi
majisafi na salama.
Kwa
upande wake mwakilishi wa (WHO) Dkt Richard Banda alisema kuwa dawa
hizo zitasaidia katika kusafisha maji na ili kusaidia jamii kupata maji
safi ya kunywa.
“WHO
tutaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutokomeza,magonjwa
yanayosababishwa na utumiaji wa maji ambayo sio salama”alisema Banda.
Comments
Post a Comment