WATU WATATU WAMEFARIKI KATIKA MATUKIO TOFAUTI MKOANI GEITA



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Mponjoli Mwabulambo akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari juu ya matukio ya mauwaji yanayoendelea kutokea Mkoani hapa.
Mtendaji wa Kata ya Bugulula Juma Choma akielezea namna walivyofanya msako wa kumsaka marehemu.

Baadhi ya waendesha piki piki wakiwa katika hali ya majonzi kutokana na msiba wa Boda boda mwenzao.

Mwili wa marehemu Mabula Sikitiko ukiwa umehifadhiwa katika shuka ukisubilia wataalam kwaajili ya uchunguzi.

Wananchi wakiwa na siraha za jadi baada ya kufanya msako wa kumtafuta marehemu katika pori la nyakabale.

Wasamaria wema wakiuwifadhi mwili huo kwaajili ya kwenda kuzikwa .



GEITA:Mkazi mmoja wa kijiji na kata ya Bugulula, Mabula Sikitiko mwenye umri wa miaka 18 dereva wa boda boda  amekutwa ameuwawa na watu wasio julikana katika pori lililopo mpakani mwa kijjiji cha Nyakabare na Nyawilimilwa Wilayani Geita.
Amekutwa akiwa ameuwawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na watu ambao bado hawajajulikana na kisha kuibiwa pikipiki yake yenye namba za usajili MC.208 AWU.

Aidha baadhi ya wanakijiji katika kijiji hicho,wamesema kuwa kutokea kwa tukio la namna hiyo ni mara ya pili tangu kutokea na kwamba paka sasa bado hawajajua ni akina nani ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya namna hiyo ambavyo ni vya kinyama.

Kamanda wa polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo,huku akitoa wito kwa waendesha pikipiki kuwa makini na kuachana na dhana ya kubeba watu wawili katika boda boda kwani dhana hiyo imeendelea kuwaangamiza wengi.

Hata hivyo kabla ya kifo hicho tarehe 22 mwezi huu majira ya saa 8:00 asubuhi marehemu akiwa Bugulula alikokodiwa na watu wawili wasiojulikana ambapo hakurudi tena hadi mwili wake ulipokutwa umetelekezwa porini.
Chanzo cha mauaji hayo ni kuwania mali,jeshi la polisi linaendelea na msako ili kuwabaini na kuwatia hatiani waliohusika na mauajihayo.
Kamanda pia ametaja matukio mengine ya kuuwawa kwa watu katika mazingira tofauti ni pamoja na tukio la tarehe 20 mwezi huu majira ya saa 11:30 jioni katika mgodi wa dhahabu wa Geita uliopo kata ya mtakuja  mkazi wa mtaa wa Nyakumbu Chacha Gailigi(30) kabila mkurya ,mkulima alifariki Dunia baada ya kudumbukia  ndani ya shimo la maji ambalo limo ndani ya mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) Tarehe 22 mwezi huu mwili wake ulionekana ukielea ndani ya maji na kuopolewa.

Kamanda ameeleza chanzo cha tukio hilo ni kuwa Tarehe 20,mwezi huu marehemu akiwa na Nelson Busumabu,waliingia kwa jinai mgodini hapo na walioonwa na walinzi wa mgodi huo walianza kukimbia ili wasikamatwe na marehemu alivua viatu pamoja na shati na kujirusha ndani ya shimo hilo la maji huku mwenzake akiendelea kukimbia na kufanikiwa kuwatoroka walinzi hao.

Kamanda ametoa rai kwa wananchi wanaopenda kuingia mgodini hapo kwa lengo la kutenda uharifu kuacha mara moja ili kuepusha madhala ambayo yanaweza kuwapata.

Comments