Judith Ferdinand, Mwanza
Jamii hasa vijana wemeombwa kuacha kutumiwa na wanasiasa kama daraja kwa ajili ya kujinufaisha wenye na kumuacha Rais John Magufuli kuinyoosha nchi iliyokuwa imefikia pabaya.
Hayo yalisemwa jana na Jijini Mwanza na aliyekuwa Katibu wa Chadema mkoa wa Mwanza na Mjumbe Mkutano Mkuu Taifa, John Nzwalile, wakati akizungumza na waandishi wa habari, juu ya msimamo wake kuhusu oparesheni Ukuta.
Aliwaomba vijana wa mkoa wa Mwanza wasikubali kutumia na viongozi wa siasa wanaoanda oparesheni za ovyo ovyo ikiwemo Ukuta kwa ajili ya kujinufaisha kwa kupata umaarufu kisiasa na kutoka kuharibu amani na maendeleo ya taifa.
Pia alisema, haikubaliki vijana na jamii kutumia katika mambo ya ovyo badala ya kujenga taifa, hali ambayo ni dhambi inayowatafuna wanasiasa kwani wakipata madhara wanaachwa bila msaada wowote.
Hata hivyo alisema,anafurahishwa na utendaji kazi wa Dkt. Magufuli kwa kuyafanyia kazi yale yote waliokuwa wanayapigania wapinzani kwa kiwango ambacho wasingeweza kufanya hasa ufisadi na watumishi hewa, hivyo anawashangaa wale wanaombeza.
"Nawashangaa wale wote wanaomuita Dkt.Magufuli kuwa ni dikteta uchwara, kwa ajili ya kupigania maendeleo ya wananchi na kuwabana mafisadi,mimi nawaita wao ndio wanasiasa uchwara ambao wapo kwa maslahi yao binafsi," alisema Nzwalile.
Aidha alisema, kuanzia sasa yeye siyo mwanachadema na anajivua vyeo vyote alivyokuwa navyo ndani ya chama hicho, ila atabaki kama shabiki wa CCM mpaka pale atakapoamua kuwa mwanachama wa chama hicho.
Vilevile alisema, atazunguka mkoa mzima wa Mwanza kuwaeleza ukweli juu ya Chadema ambayo wanadhani ni nyeupe kumbe nyeusi kwa kuanika maovu yanayofanywa na chama hicho
Comments
Post a Comment