WAZIRI LUKUVI: SERIKALI TUMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

Waziri wa Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
Na Sheila Simba- MAELEZO

Waziri wa Aridhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa Serikali imeanza kazi ya kupima
ardhi  nchi nzima kuanzia mkoani
Morogoro.

Akizungumza  katika kipindi kipya cha
"TUNATEKELEZA" kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO na TBC1
,alisema utekelezaji wa zoezi hilo umeanzia mkoani humo ili kupima maeneo ya
wakulima na wafugaji na kutatua migogoro ya ardhi Mkoani humo.

“Serikali tumedhamiria
kumaliza migogoro ya ardhi, kutimiza ndoto ya Rais Magufuli ya kuondokana na
migogoro ya ardhi isiyo na tija inayosababisha watu kupoteza maisha’’Alisema
Lukuvi

 Ameongeza kuwa katika upimaji huo wa ardhi
serikali inashirikiana na kampuni binafsi zilizosajiliwa ili kumuwezesha
mwananchi anayemiliki shamba,kiwanda ,mkulima na mfugaji mwenye eneo  kupimiwa na kuongezewa thamani.

 “Nakuhakikishia katika kipindi cha miaka 10
kila kipande cha ardhi Tanzania kitakuwa kimepangwa na kupimwa utaratibu mzuri
utakao mwezesha kila mtumiaji wa ardhi kutumia eneo lake”alifafanua Lukuvi.

Pia ameeleza suala la
kuthibiti bei ya kupima ardhi kwa kushirikiana na wapimaji binafsi katika
kumfanya kila mtanzania alipe bei halali ya kupima ardhi.

Aidha amesme kuwa Serikali
itaweka ukomo wa kumiliki ardhi ili kuondoa tabia za watu kumiliki eneo kubwa
la ardhi bila ya kuliemdeleza kwa muda mrefu.
“serikali itaweka muda wa
mtu kumiliki ardhi, haiwezekani mtu mmoja amiliki eneo hata bila kulitumia,
tabia hii itafika mwisho.”

Akizungumzia suala la wageni
kumiliki ardhi alisema kuwa ni marufuku kwa wageni na wawekezaji kununua ardhi
vijijini bila kupitia wizara inayohusika.

“Ni marufuku kwa mgeni au
mwekezaji kwenda kijijini kununua ardhi bila kuja kwangu au Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC),wakifanya hivyo tutawapa ardhi wawekeze, Pia mtu yeyote
anayetaka kujenga kiwanda popote afike ofisini kwangu nitampatia ardhi ndani ya
siku saba.”alisema Lukuvi

Ameongeza kuwa  Wizara imetenga viwanja 240 kwa ajili ya
Viwanda enoa la Kigamboni ili kutimiz lengo la Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa
viwanda.

Mbali na hayo Waziri Lukuvi
alisema  wananchi wote waliodhulumiwa
viwanja Jijini Dar es Salaam kwa makosa ya watendaji wa Serikali wameanza
kupewa  viwanja vingine mbadala.

“Naagiza Halmashauri zote
ziwapatie viwanja mbadala wananchi ambao walidhulimiwa viwanja vyao kwa makosa
ya watendaji.”


MWISHO

Comments