Walimu wa Ushirombo Sekondari wakutana na Mbunge Doto

Baadhi ya Majengo ya Shule ya Sekondari Ushirombo.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko,Viongozi wa Idara ya elimu ngazi ya Kata na Wilaya wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Shule ya Sekondari Ushirombo.

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na Walimu wa Shule ya Sekondari  Ushirombo

Picha ya baadhi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Ushirombo wakimsikiliza Doto Mashaka Biteko(Mb) katika ofisi ya walimu shuleni hapo.

 Picha ya Pamoja baada ya mazungumzo shuleni hapo.



Mbunge wa jimbo la Bukombe mkoani Geita, Mhe .Doto Mashaka Biteko
amewachagia kwenye mfuko wa jamii kiasi cha shilingi laki tatu ili kuutunisha mfuko huo wenye niaba ya kusaidiana kwenye maafa na sherehe kwa walimu shuleni hapo.

 Kabla ya Mbunge kuchangi mfuko huo  wa maendeleo ulioibuliwa na mmoja wa walimu shuleni hapo Mhe. Biteko aliwashukuru kwa kumchagua siku ya uchaguzi Oktoba 25 mwaka 2015 na kwamba hawezi kumlipa mmoja mmoja kwa  kazi yake aliyoifanya na kusema  atahakikisha anawatumikia na kuwatetea walimu na wananchi kwa ujumla wa Bukombe ili wapate maendeleo.

Aidha katika mazungumzo hayo  walimu waliorodhesha changamoto zao ikiwa ni ukosefu wa miundo mbinu ya umeme,samani za ofisini ikiwa ni sambamba na kukaa kwenye ofisi ndogo hali inayo wasabishia wengine kukaa nje ya ofisi hiyo kulingana na mbanano iliopo,wanafunzi kukosa nidhamu kwa walimu hali inayowaatarishia kushuka kwa taaluma  shuleni hapo na kutokulipwa na serikali madai yao hali anayo wasababishia kuvunjika moyo wa kuendelea kufanya kazi.

Kwa upande wake Mhe. Biteko wakati akiwapongeza walimu kwa kujuhudi wanazozionyesha na kuzifanya juu ya kuinua kiwango cha elimu shuleni hapo  aliwaomba walimu hao kushirikiana kwa karibu sana na wazazi kuhakikisha suala zima la nidhamu kwa wanafunzi linarejea kwa kasi kwani kila mwanafunzi anatoka kwenye jamii ya tofauti na ya mwenzake.




Comments