Namsega Fc yapata Ushindi wa tatu katika Ligi ya Doto Cup-Bukombe

 Wachezaji wa Timu ya Katome Fc wakiwa wameduwa baada ya kufungwa gori.
 Baadhi ya mashabiki wakishuhudia mechi katika uwanja wa Kilimahewa.



Timu ya Namsega  imeweza kuifunga timu ya Katome Fc katika  hatua ya nusu fainali na kuibuka mshindi wa tatu wa Ligi hiyo ya Doto Cup baada ya kichapa gori 4-0 timu ya Katome Fc  katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Halmashauri ya Bukombe uliyoko  Kilimahewa Mjini Ushirombo  Wilaya ya Bukombe Mkoani  Geita.
Katika hatua ya nusu fainali hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya mashabiki Timu ya Namsega ilijipatia gori la kwanza dhidi ya Timu ya Katome Fc dakika ya 13,dakika ya 76 gori la pili na dakika ya 85 gori la tatu kupitia kwa kiungo mshambuliaji Robert Kalimana na kufanikiwa kuongeza tena gori la nne kupitia kwa mchezaji Viti Kabili kunako dakika ya 90.
Hadi dakika ya tisini ya mchezo huo Timu ya Katome haikufanikiwa kupata hata gori lakufutia chozi.


Comments