TIMU YA UYOVU FC YAIADABISHA KATENTE FC KATIKA LIGI YA DOTO CUP.




Ikiwa ni mwedelezo wa Ligi ya Doto Cup ngazi ya Wilaya baada ya kushindana Vijiji kwa Vijiji, Kata kwa Kata, Tarafa kwa Tarafa,Timu ya Uyovu Fc iliyopo  Kata ya Uyovu Wilayani Bukombe Mkoani Geita jana ilifanikiwa kuichapa gori 4-2 Timu ya Ketente Fc katika hatua ya mzunguko wa kwanza wa Ligi hiyo ngazi ya Wilaya.
Mechi hiyo iliyohudhuliwa na mamia ya mashabiki katika uwanja wa Halmashauri ya Bukombe ulioko Kilimahewa Kata ya Katente
 Timu ya Uyovu Fc iliichapa gori 4 Timu ya Katente Fc ikiwa ni dakika ya 8 kwa mchezaji Welason Ramadhani mwenye jezi namba 10,gori la pili na la nne lilifungwa na kiungo mshambuliaji Rashid Suleiman mwenye jezi namba14 ikiwa ni dakika ya 13 na 73 nala tatu kufungwa na mchezaji Ramadhani Unus mwenye jezi namba 8 dakika ya 23

Kwa upande wao Katente Fc katika harakati za kujikwamua walipata magori mawili kupitia kwa mchezaji Matendo Ngai mwenye jezi namba 4 dakika ya 18 na dakika ya 38 kujipatia gori la pili kupitia kwa kiuongo mshambuliaji Lenard Kumuhu mwenye jezi namba 9 hadi dakika ya tisini jitihada zao zilikomea hapo na kukubali matokeo.

 Akizungumza baada ya mechi kumalizika,  Katibu wa Chama cha Mpira Wiayani Bukombe (BUFA) Mwl Kabalega amezipongeza timu zote zilizojitokeza kushiliki ligi hiyo  iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa lengo la kuendeleza vipaji vya vijana wanaopatikana ndani ya jimbo la Bukombe. 

Comments