Sherehe ya kupongeza shule mbili za msingi na moja ya sekondari Tarafa ya Siloka-Bukombe


Picha ya baadhi ya walimu wa Tarafa ya Siloka waliofaulisha vizuri wakiwa katika hafla ya kupongezana.

Baadhi ya wadau wa elimu wa Tarafa ya Siloka waliochangia kufanikisha hafla hilo.

Hawa ni waalimu waliotunukiwa vyeti  katika Sherehe hiyo.

 
Walimu wa shule mbili za msingi na Sekondari moja tarafa ya
Siloka  Wilayani Bukombe Mkoani Geita,watunukiwa vyeti vya ufaulu
masomo mbalimbali wakuu wa shule wakipewa vyeti vya uongozi bora kwa
kufanya vizuri katika matokea ya darasa la saba 2015/16 na kidato cha
sita.

Katibu tarafa ya Siloka Tumbo  Madaraka ambaye alikuwa mwenyekiti wa
hafla hiyo ya kuwapongeza walimu hao alisema kuwa walimu hao wana haki
ya kupongezwa kwa kazi nzuri walio ifanya katika matokeo ya mwaka
2015/16.

Madaraka alisema walimu wa shule zilizo fanya vizuri kila mwaka
atahakikisha anaada mda wa kuwapongeza na kutoa motisha kwao ili
kuwapa moyo wa kujituma katika uajibikaji na kuhakikisha wana fanya
mashindano ya kufaulisha.


Awali mkuu wa shule ya msingi Uyovu Severin Jegu alisema shule imekuwa
ikifanya vizuli tangu 2013/2014/ na 2015 ilishika nafasi ya kwanza
katika wilaya kati ya shule 78 alisema wanafunzi walio fanya mtihani
wa kumaliza darasa la saba  wavulana 30 wasichana 33 nawote walifaulu
kwa asilimia 100 shule inaupugufu wa madarasa 38 huku upungufu wa
madawati 314 yaliyopo 200.


Mkuu wa shule ya msingi Ibamba Thobias Mkalanga alisema wanafunzi
walio faulu mwaka 2015/16 wanafunzi 68 walifaulu na kuifanya shule
hiyo kushika nafasi ya nne kiwilaya ya pili kitarafa alisema ufaulu
kimadaraja A- wavulana 8 wasichana hakuna B- wavulana 25 wasichana 24
C- mvulana mmoja wasichana 10 msicha mmoja hakufanya mtihani waliokuwa
wamesajiliwa ni 69.

Mkalanga alisema shule hiyo inachangamoto upungufu wa walimu kutokana
na wanafunzi kufikia 3160 darasa la awali hadi lasaba  wavulana 1518
wasichana 1642 huku walimu waliopo 19 tu hawapo 51  mahitaji ya nyumba
za walimu 70 hakuna hata moja na inauhaba wamadawati.


Naye mkuu wa Shule ya sekondari Runzewe Renatus Bahathi alisema ufaulu
kidado cha sita 2015/16 wanafunzi 150 wavulana wote  kidado cha sita
walifaulu wote daraja la kwanza 48 daraja la pili 42 daraja la tata 20
daraja la nne hakuna hata sifuli hakuna ufaulu asilima 100 na kushika
nafasi ya kwanza wilaya na mkoa kitaifa nafasi ya 27 kati ya shule
423.

Bahati alisema shule hiyo imekuwa ikifanya vizuli tangu 2013 na
2015/16 wanafunzi kidato cha  sita Elikana Simon alikuwa wa tatu kati
ya 10 bora waliofanya vizuri kitaifa kwa masomo ya sanaa na lugha
katika mitihani ya taifa kidato cha sita 2016 .

Alisema ufaulu huo ambao umechagiwa na mikakati mbali mbali utowaji wa
motisha kwa walimu na wanafunzi, usimamizi wa nidhamu, kujituma,kuweka
vikundi vya kusoma wanafunzi,mkuu wa shule  alisema wanakabiliwa na
ukosefu wa kisima kirefu cha maji ukosefu wa maktaba kwa ajili ya
kutunza vitabu kujisomea na utafiti upungufu wa vitabu vya somo la
sayansi.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Bukombe Dionis Myinga kwa niamba
ya Mkuu wa Wilaya Josephat Maganga ambaye alikuwa mgeni rasmi, Myinga
aliwapongeza walimu na kuwakabidhi vyeti  kwa walimu wa kawaida na
wakuu wa shule kupewa vyeti vya uongozi bora.

Myinga aliwaomba walimu kuwa wavumilivu wakati serikali kiendelea
kuweka utalatibu wa kupunguza changamoto zinazo kabili mashuleni
nakwamba kitendo kilicho fanywa na katibu tarafa kimemvutia atafanya
kiwilaya kutowa motisha kwa walimu.


Comments