Baadhi ya wanakikundi cha Runzewe Development Group(R.D.G) na Igunanilo wakimsikiliza
Mwenyekiti wao Dr. Baraka Charles Kulwa walipokuwa ikizungumza wakati wa kukabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Bwn Josephat Maganga.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Bwn. Josephat Maganga,Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko,Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na baadhi ya Madiwani wakisikiliza risala kutoka kwa wanakikundi cha Runzewe Development Group(R.D.G) na Igunanilo ikiwa ni hatua ya kujua nini hatua walizonazo, malengo yao na changamoto kwa vikundi hivyo.
Mmoja wa wanakikundi hao akikabidhi risala kwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Bw. Josephat Maganga baada ya kuisoma.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza katika makabidhiano hayo ya madawati
Mwenyekiti wa Kikundi cha Runzewe Development Group(R.D.G) na Igunanilo Group Dr. Baraka Charles Kulwa na mmoja wa wanakikundi hao Mwl Ndizu wakiwa wamebeba dawati kama ishara ya kumkabidhi madawati hayo kwa niaba ya wanakikundi wenzao kwa Mkuu wa Wilaya ya BukombeBw. Josephat Maganga.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Bw. Josephat Maganga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bukombe Dionis Myinga wakiyatazama madawati baada ya kukabidhiwa.
.
Picha ya Pamoja baada ya makabidhiano ya Madawati.
Baada ya upungufu wa madawati Wilayani Bukombe Mkoani Geita, vikundi vya
Runzewe Development Group(R.D.G) pamoja na Igunanilo Group vimemkabidhi Mkuu waWilya ya Bukombe madawati 63 ikwa ni hatua ya kupunguza changamoto ya shule zinazo kabiliwa na upungufu wa madawati wilayani Bukombe.
Akizungumza Mwenyekiti wa vikundi hivyo Dr. Baraka Charles Kulwa amesema
anamshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko
kwa hamasa alizozifanya wakati akizunguka jimboni kwake kwenda
kuhamasisha maendeleo na kuviomba vikundi na taasisi vilivyo na uwezo
kujitokeza kuchangia madawati ili kupunguza changamoto zilizoko kwenye
shule za msingi na sekondari katika Wilaya ya Bukombe.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko amesema kuwa suala la huduma za kijamii ikiwemo Elimu na Afya siyo la
Serikali pekee hivyo ni vyema jamii ikatambua pia inao wajibu wa
kushiriki na kuchangia katika kufanikisha upatikanaji wa huduma hizo
muhimu.
Mkuu wa Wilaya Bukombe Bwn. Josephat Maganga amewashukuru wadau hao kwa kuguswa na kujitoa kwa hali na mali ili kufanikisha zoezi la uchangiaji wa madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi Wilayani Bukombe.
Comments
Post a Comment