Namsega Fc yapata Ushindi katika Ligi ya Doto Cup-Bukombe August 13, 2016 Get link Facebook X Pinterest Email Other Apps DOTO CUP Timu ya Namsega imeweza kuvuka hatua ya 8 bora michuano ya kombe la Doto Cup baada ya kuifunga goli 1-0 timu ya Buntubili katika mechi ya kwanza iliyochezewa katika uwanja wa Halmashauri ya Bukombe ulioko Kilimahewa mjini Ushirombo Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita . Mechi ya kwanza ya timu hizo iliyochezwa Mechi hiyo iliyohudhuliwa na mamia ya mashabiki katika uwanja wa Kilimahewa Timu ya Namsega ilichapa gori 1 Timu ya Buntubili Fc dakika ya 68 kupitia kwa kiungo mshambuliaji Richard Bitungwa. Hadi dakika ya tisini ya mchezo huo Timu ya Buntubili fc haikupata hata gori la kufutia chozi. Kipa wa Buntubili Fc Isa Unusi "Degea" ndiye aliyekua nyota wa mchezo kwa kuokoa mipira mingi ya hatari likiwemo shuti la Marco Mwenye Jezi namba 10 alilopiga ndani ya 18 na kipa huyo wa Butubili kuokoa kwa mguu. Comments
Comments
Post a Comment