Mwenyekiti wa Wazazi CCM Mkoa wa Geita afanya ziara Chato.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Geita na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisalimiana na wajumbe wa Jumuiya hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Chato kwa Mkutano wa ndani.

Hivi ni baadhi ya vikundi vilivyotoa burudani katika mkutano huo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Geita na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko na Katibu wa CCM wa Wilaya ya Chato bw. Hamisi Mkaruka wakifuatilia burudani zilizokuwa zikiendelea.

  Katibu wa CCM wa Wilaya ya Chato bw. Hamisi Mkaruka akizungumza katika mkutano wa Jumuiya ya Wazazi Wilayani Chato.


 Timu ya vijana inayofadhiliwa na Jumuiya ya Wazazi CCM-Chato inayoitwa WAZAZI FC
 
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Geita na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akumkabidhi mmoja wa vijana wachezaji Kadi ya Jumuiya hiyo.


Katibu wa Elimu,Malezi,Uchumi na Mazingira-Chato Bw. Ramso Sababu Ndaki akiwaapisha baadhi ya vijana waliopewa Kadi za Jumuiya hiyo baada ya zoezi la kupewa Kadi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Geita  Mhe. Doto Mashaka Biteko.
  
Kaimu  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Chato bw.Sebastiani Kabilima akifungua mkutano huo katika Ofisi ya CCM-Chato.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Geita na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wajumbe  baada ya kukaribishwa

 Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato wakimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Geita na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.

Picha za wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Geita na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko katika mkutano uliofanyika kwenye Ofisi Kuu ya CCM Wilaya ya Chato .
 
Akizungumza na wajumbe hao ameanza kwa kuwapongeza kwa mahudhurio yao na kuwazawadia mipira miwili na chezi pea mbili timu ya Wazazi Fc ikiwa ni hatua ya kuinua vipaji kwa vijana hao.

Katika hatua nyingine Mhe. Doto Mashaka Biteko amewafikishia salaam nyingi kutoka kwa Mbunge wao Mhe. Medard Kalemani na kueleza kuwa Mbunge huyo alitamani na yeye  awepo katika mkutano huo ila kulingana na majukumu haikuwezekana.

Pia Mhe. Doto aliwasihi wajumbe wa jumuiya hiyo kushikamana,kushirikiana,  kupendana na kufanya kazi kwa bidii ya kuimarisha Chama na kutoa ada kwa wakati ili wawe hai kwani kiwango cha ada ni kidogo haina maana ya kuacha kujihuisha.

Na kuongeza kwa kusema kuwa kwa sasa maadili ya vijana yameshuka hivyo waone ni jukumu lao kwa pamoja kusimamia suala zima la nidhamu ili kuliokoa Taifa na kuunnga mkono Serikali kwa kumsaidia raisi wetu kwa nguvu na umoja wetu bila kujali dini, kabila wala itikadi za vyama.  

Comments