Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Geita ahitimisha ziara yake ya siku 5 Chato,Geita Mjini,Nyang’wale,Mbogwe na Bukombe.


Ofisi ya Kuu ya CCM ya Wilayani Bukombe.

Zahanati ya Luganga-Bukombe aliyozinduliwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Mkoa wa Geita Mhe. Doto Mashaka Biteko.

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Mkoa wa Geita Mhe. Doto Mashaka Biteko akikata utepe kwa ajili ya ufunguzi.

 Zahanati ya Dillu-Katente aliyozinduliwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Mkoa wa Geita na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.

Sehemu ya Kuchomea taka.
   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Mkoa wa Geita Mhe. Doto Mashaka Biteko akikata utepe kwa ajili ya ufunguzi wa Zahanati ya Dillu.

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Mkoa wa Geita na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya wazazi wa Wilaya ya Bukombe.

Picha ya Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Bukombe wakimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Mkoa wa Geita na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Geita na Mbunge wa jimbo la Bukombe mkoani Geita Doto Mashaka Biteko
amefanya zoezi la ufunguzi wa Zahanati mbili zinazodhaminiwa na Jumuiya hiyo ya Wazazi ambazo ni Zahanati ya Luganga na Zahanati ya Dillu zilizoko katika Kata ya Bukombe na Katente Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.

Akiwa anahitimisha ziara yake Wilayani  Bukombe  baada ya kuzunguka Wilaya zote za Mkoa wa Geita  Mwenyekiti huyo na Mbunge aliwapongeza sana Jumuia ya Wazazi kwa kitendo cha kusaidia kusogeza huduma za Afya kwa   jamii kwa kusaidia kupunguza  vifo visivyo vya lazima hasa kwa Wamama na watoto katika Wilaya hiyo ya Bukombe.

Biteko wakati akiwapongeza wanajumuiya hiyo kwa kuibua huduma za kuwanusuru uhai wananchi  kwa kujenga Zahanati hizo aliwataka wanajumuiya kushirikiana kwa karibu zaidi na wataalamu wa zahanati hizo na kuwasihi Viongozi wa Jumuiya hiyo ya wazazi kutowabugudhi wataalamu hao wa afya kwa kuwaomba rushwa ili kuwapa mwanya wa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Geita na Mbunge  wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko  alipokuwa  ikizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi CCM wa Wilaya ya Bukombe aliwasihi wanajumuiya na wanachama wa CCM kushirikiana kwa karibu na viongozi ili kuleta maendeleo kwa kasi,kuongeza upendo kwa chama na wanachama  kwa ujumla, kuthaminiana na kuhudumiana kwenye matatizo ya kijamii na kuhusika moja kwa moja kwa kushirikia na serikali ili kujiletea maendeleo bila kujali itikadi zetu dini wala ukabila kwa kuchangia madawati mashuleni ikiwa ni hatua ya kumuunga mkono raisi wetu anaetoa elimu bure na kuibua miradi ya maendeo mara kwa mara.

Pia alissisitiza sana suala la malezi ya watoto na kusema ”Kwa sasa maadili ya watoto wetu yameshuka hivyo tuwe mstari wa mbele kuhakikisha nidhamu ya watoto wetu inaimarika ili kulinusuru taifa letu” Alisema Mhe. Doto.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wa Wilaya ya Bukombe bw.Mhangwa Butachaga aliwashuwashukuru sana wajumbe kwa umoja waliouonyesha wa mwitikio wa Mkutano kwa kuwa na mahudhurio makubwa na kuwasihi waendelee hivyohivyo ili kujenga chama na serikali madhubuti daima.

Comments